Kufuatia
idadi kubwa ya Watanzania ambao mara kwa mara husafiri kwenda India kwa sababu
tofauti tofauti za kimatibabu, wataalamu kutoka Hospitali ya Apollo, Hyderabad, wamefikia uamuzi wa kutoa tiba na ushauri
wa kitaalamu kwa Watanzania kupitia kiliniki maalumu ya siku mbili itakayofanyika
Dar es Salaam. Kliniki hii maalum itaendeshwa na mtaalamu wa upasuaji wa
mfumo wa fahamu, Dkt Alok Ranjan na mtaalamu
wa upasuaji wa mifupa, Dkt Somasekhar Reddy katika hospitali ya Hindu Mandal tarehe 27 na 28 Aprili.
Timu hiyo
ya madaktari wataalamu kutoka Hospitali ya Apollo itaambatana na Bw. Radhey Mohan makamu mwenyekiti, maendeleo
ya biashara kimataifa katika hospitali ya Apollo Hyderabad. Tukio hili la
siku 2 itakuwa fursa ya watu wenye magonjwa yanayohusiana na magoti, nyonga,
mabega na mfumo wa fahamu kuonana na madaktari wanaotambulika kimataifa kwa
uchunguzi wa awali na ushauri.
Makamo wa
rais anasema “Kwa sasa Idadi ya
Watanzania wanaotafuta huduma za afya nje na hasa India ni kubwa, kila siku
tunapokea watu wanaohitaji huduma zenye ubora wa hali ya juu. Kuzingatia hili
tumeamua kutanua wigo wetu na kufikisha wataalamu wetu karibu na wahitaji ambao
wanaweza wasipate fursa au namna ya kuonana nao”. Kulingana na Bw. Radhey Mohan hatua hii ni alama ya
mahusiano ya muda mrefu ambayo hospitali za Apollo zimeanzisha na Tanzania
ambapo kwa miaka mingi imeshuhudia hospitali hizi zikitoa huduma zake kwa
waathirika wa magonjwa mbalimbali yaliyokithiri nchini.
Kliniki
hii ya siku mbili itawahudumia wagonjwa mbalimbali na ipo wazi kwa kila mmoja
atakayewahi kuweka miadi; wagonjwa hawa watafanyiwa uchunguzi, watapewa maelekezo
na ushauri wa kitaalamu kwa kuzingatia matatizo waliyonayo.
Akiwa na
uzoefu wa zaidi ya miaka 25, na akiwa amekwishafanya upandikizaji wa viungo
zaidi ya mara 1,000, Dkt Somasekhar
Reddy, Mshauri mwandamizi wa upasuaji wa mifupa, Hospitali ya Apollo, Hyderabad,
atawahudumia watu wenye matatizo yanayohusiana na magoti, nyonga na mabega. Dkt Reddy ana uzoefu wa juu katika
kufanya kazi karibu zaidi na Watanzania waliokumbwa na matatizo yaliyotajwa
amekwishawafanyia upasuaji zaidi ya Watanzania 200 katika kipindi cha miaka 7
hadi 8.
Dkt. Reddy anaongoza timu ya
wataalamu upasuaji wa mifupa ambayo inatoa huduma za kipekee kwa matatizo yote
ya mifupa na viungo katika hospitali ya Apollo. Utaalamu wake hasa ni katika
kupandikiza nyonga, goti na bega, upasuaji wa kupandikiza nyonga, upasuaji wa
goti, upasuaji usio vamizi, majeraha katika
maungio ya goti na bega pamoja na upasuaji wa kusaidia mguu wenye saratani ya
mfupa.
Atakayeambatana
na Dkt Reddy ni Mkuu wa kitengo cha upasuaji wa mfumo wa fahamu katika hospitali ya
Apollo, Hyderabad Dkt Alok Ranjan ambaye kwa upande wake atahudumia
wagonjwa wanaohitaji upasuaji umakini zaidi wa mfumo wa fahamu. Ni mkongwe
katika upasuaji usio vamizi wa uti wa mgongo na
saratani ya ubongo, upasuaji mdogo wa mfumo wa fahamu akiwa ameweka rekodi ya
kufanikiwa kutibu zaidi ya wagonjwa Watanzania 1,000 kwa kipindi cha miaka 10
iliyopita kwa matatizo magumu ya ubongo na uti wa mgongo.
Dkt Ranjan ni mtaalamu katika
upasuaji wa fuvu lenye saratani, upasuaji tata wa uti wa mgongo, upasuaji kwa
watoto wadogo, upasuaji unaohusisha mionzi, upasuaji wa mfumo wa fahamu
ujulikanao kitaalamu kama AVM, upasuaji kwenye ubongo kwa kutumia hadubini,
upasuaji kwa wagonjwa wa kifafa na ule wa kuusisimua ubongo.
Watanzania wanahamasishwa kutumia fursa hii kuwaona
madaktari na kupata ushauri wa awali wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wanaotaambulika
kimataifa. Ushauri huu wa siku mbili utafanyika hospitali ya Hindu Mandal Dar
es Salaam tarehe 27 na 28 Aprili kati ya saa 3 asubuhi na saa 12 jioni. Kwa
watakohitaji kuweka miadi na madaktari wanaweza kupiga simu +255 682 052 342 or +255 22 211 499-4.
Kuhusu
Hospitali ya Apollo
Hospitali ya Apollo imefanikiwa
kupata kibali cha bodi ya Kimataifa((JCI) iliyopo Marekani bodi yenye lengo la kuboresha
ubora wa huduma ya afya na usalama duniani kote. Kibali cha kimataifa cha dhahabu
kwa ajili ya hospitali. Tofauti ya kipekee ya kufikia kibali kwa ajili ya
hospitali hiyo kuanzia Delhi, inakuwa hospitali ya kwanza nchini India kupata vibali
hivyo mfululizo kwa mara ya nne, wakati hospitali ya Apollo Chennai, ikiwa
hospitali ya kwanza kusini mwa India kupata kibali hiki cha kipekee.
Hospitali hii ni kituo bora katika
huduma za saratani. Ina mtandao wa tiba ya kansa ambao ni mtandao mkubwa sana
nchini India. Unaotoa huduma ya Saratani ikiwa ni pamoja na kinga na tiba .Yenye vifaa na hali
nzuri ya teknolojia kama vile upasuaji kwa kutumia Roboti, PET CT Scanner, Tumour
board na hivi karibuni wameongeza NovalisTx, kiwango kipya katika tiba ya
mionzi na upasuaji, Inatoa huduma ikiwa ni pamoja na mionzi ya saratani, madawa
ya saratani,upasuaji,pamoja na Kliniki ya kitaalamu kwa ajili ya saratani ya
matiti, Saratani ya kichwa, mdomo na koo.
Uchunguzi wa wakatini muhimu kwa
mafanikio ya tiba, hospitaliya Apollo inatoa huduma ya uchunguzi wa Saratani,
ambayo ni pamoja na uchunguzi maalum wa kijinsiaunaogusa saratani zote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)