Dar es Salaam: Mwezi Machi sekta ya afya nchini Tanzania imepokea
wataalam kutoka nchi mbalimbali duniani
kwa ajili ya kutoa huduma za vipimo, ushauri na matibabu kwa watanzania. Ujio
huu umeleta faida kubwa kwa wagonjwa na wataalamu nchini. Miongoni mwa waliotembelea
ni timu ya Madaktari bingwa kutoka
Israel na Hospitali za Apollo zilizopo nchini India. Ziara hizi za mwishoni mwa
mwezi March zilitanguliwa na ziara ya madaktari wawill kutoka hospitali ya
Apollo ya bangarole mwanzoni mwa mwaka huu.
Ikiwa
tayari walifanya kliniki ya ushauri kwa ajili ya wagonjwa wa figo na mfumo wa fahamu timu ya wataalam kutoka hospitali ya Apollo
Bangalore ilirudi Tanzania kwa ajili ya uchunguzi na kutoa ushauri zaidi kwa wagonjwa wa Moyo na mfumo wa fahamu. Kliniki hiyo ilifanyika mwishoni mwa Machi
katika hospitali ya Medi Ed jijini Dar es salaam, iliandaliwa na Dk. Girish Navasundi, dakitari mwandamizi wa magonjwa ya moyo, katika hospitali ya
Apollo ya Bangalore na Profesa Dk Krishna Kambadoor, Mkurugenzi
wa Taasisi ya sayansi ya mfumo wa fahamu kutoka Hospitali ya Apollo ya
Bangalore.
Kliniki hiyo ilitoa fursa kwa umma kupata uchunguzi wa matatizo hayo bure bila
kulipia gharama yoyote na pia kuruhusu madaktari kufuatilia maendeleo ya
wagonjwa wao ambao hawakuweza kurudi
india kwa uchunguzi na matibabu ya zaidi.
Magonjwa
yasiyo ya Kuambukiza (NCD) kama vile
moyo, mfumo wa neva na mgongo yamekua yakiongezeka
kwa kasi na kusababisha ongezeko la vifo
nchini. Akizungumza na waandishi wa habari wakati madaktari kutoka Israel
wakiwafanyia uchunguzi watoto wenye matatizo ya moyo, makamu Raisi wa chama cha madaktari wa watoto
Tanzania, Dk Namala Mkopi alizungumzia matatizo ya magonjwa ya moyo kwa jamii
na hasa kuonyesha athari zake kwa watoto wachanga na kusema kuwa inakadiliwa
"watoto 13,600 nchini huuzaliwa na matatizo
ya moyo kila mwaka na asilimia 25 tu ndio wana uwezo wa kupata matibabu. Mwaka
2013 na 2014 kati ya watoto 322 waliokutwa na matatizo, 128 tu walipata nafasi
ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi"
Wakati wa wakati wa kambi ya uchunguzi
iliyooandaliwa na Hospitali ya Apollo, Dr Girish B Navasundi dakitari mwandamizi wa magonjwa ya moyo,
katika hospitali ya Apollo ya Bangalore aliwahudumia wangonjwa wenye magonjwa yanayohusiana na moyo. Dr Girish B Navasundi ni dakitari bingwa na mashuhuri kwa kuwa na uzoefu mkubwa wa miaka
kadhaa katika idara ya magonjwa ya moyo, baada ya kufanya zaidi ya matibabu ya
moyo kwa wagonjwa 1700 kwa njia ijulikanayo kitaalamu kama Angiograms. Zaidi ya
mafanikio haya pia anatambulika kwa kufanya matibabu ya moyo kwa wagonjwa 350 kwa njia ijulikanayo kitaalamu kama Angioplasties.
Katika Kambi
hiyo Dk Navasundi alikuwa na nafasi ya kuelimisha
Watanzania juu ya umuhimu wa maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa ya moyo
utamaduni ambao Watanzania wengi hawana. Alisema kuwa, "moyo hauwezi kufanya
kazi bila maji ikiwa asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Kwa hiyo, unywaji
wa maji ni muhimu kwa utendaji wa mwili,
na hasa zaidi kwa mishipa ya moyo"
"Nini
kinatokea kama mtu hata kunywa maji? Kwanza, mishipa midogo ya damu
(capillaries) katika mwili wako itafunga. Hii kuongezeka upinzani katika mzunguko
wa damu na kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu. Ukosefu wa maji huongeza hatari kwa moyo, kushindwa kwa mshipa ya damu, na matatizo mengine
yanayoendana na hayo." alisema.
"Ni
kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa? Mwili
wa binadamu unahitaji angalau ml 35 ya maji kwa kila kilo ya uzito wa mwili kwa siku , ambayo
ni sawa na ml 2100 kwa mtu wa uzito wa
kg 60. Kutumia glasi tano za maji au zaidi kwa siku kwa kiasi kikubwa hupunguza
mashambulizi ya moyo kwa kiasi kikubwa, ikilinganishwa na kunywa chini ya glasi
mbili za maji kwa siku "aliongeza Dk
Navasundi.
Dk Navasundi alihitimisha kwa kuelezea faida za matumizi ya
maji ya kutosha katika kufanya damu kuwa
nyepesi kama inavyotakiwa kuwa, hurahisisha mzinguko wa damu kwenda kwenye moyo,
kupungua kazi kubwa ya moyo vile kupunguza hatari ya damu kuganda ndani ya
mishipa,.
Tanzania
imekua ikifaidika na msaada kutoka jumuiya za Kimataifa, uingiaji wa madaktari
mashuhuri kutoka nje imekua si tu faida watu wanaohitaji matibabu lakini pia
wataalamu wa hapa nchini kwa sababu inawapa
nafasi ya kupata elimu ya matibabu, tukio ambalo litawanufaisha Watanzania kwa muda
mrefu.
Kuhusu Hospitali ya Apollo, Bangalore Idara ya Magonjwa
ya moyo
Idara inalenga katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa
moyo kupitia njia vamizi na zisizo vamizi
matibabu na uchunguzi unaosimamiwa na timu ya wataalamu wenye ari na nia ya
dhati. Katika idara ya hii kuna timu ya madakitari wa moyo waliojitolea ambao
wanafanya kazi sanjari na kutoa huduma kwa kina, kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na
magonjwa ya moyo. Timu ya madaktari, manesi na wataalamu wengine wa moyo wanakuwepo
kuhakikisha ubora katika huduma anayopatiwa mgonjwa.
Idara ya
magonjwa ya moyo katika Hospitali ya Apollo imeadhimia kutoa huduma ya afya ya
kiwango cha kimataifa kwa gharama nafuu. Timu yenye utaalamu ya madakitari
bingwa wa moyo pamoja na teknolojia ya
kisasa huhakikisha huduma bora kwa wigo mpana wa magonjwa ya moyo.
Pia kuna
idara inayohusika na matatizo ya moyo
kwa watoto pekee (ikiwa ni pamoja watoto ambao bado hawajazaliwa), waliozaliwa
na wanaokua. Miundo, kazi, na matatizo yanayohusiana na magonjwa ya moyo hushughulikiwa kwa mafanikio ya hali ya juu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)