Garissa Attack:Serikali ya Kenya yamtambua muuaji - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Garissa Attack:Serikali ya Kenya yamtambua muuaji

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wakitoroka shambulio
Serikali ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa Abdirahim Abdullahi ni miongoni mwa watu wanne walioshambulia chuo kikuu cha Garissa siku ya alhamisi na kuwaua watu 148.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kazkazini mashariki mwa kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages