Fifa yatoa viwango vipya vya soka . - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Fifa yatoa viwango vipya vya soka .

Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetoa viwango vipya vya soka duniani huku Tanzania na Rwanda zikishuka kwa nchi za Afrika ya Mashariki wakati Kenya, Uganda na Burundi zikipanda viwango.
Kushuka na kupanda kwa viwango kunatokana na mechi za kirafiki za kimataifa za Fifa zilizofanyika mwezi Machi , ambazo matokeo yake ni sehemu ya kigezo.
Tanzania, baada ya kutoka droo ya 1-1 na timu ya Malawi katika moja ya mechi hizo za kirafiki, imeshuka kutoka nafasi ya 100 mpaka ya 107 huku Rwanda ikishuka nafasi 10 hadi ya 74 baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Zambia cha magoli 2-0 mwezi Machi.
Uganda ndio nchi inayoongoza katika Afrika ya Mashariki ikipanda nafasi mbili juu na kushika nafasi ya 72 baada ya kuwafunga Nigeria 1-0.
Burundi nayo imepanda kutoka nafasi ya 126 mpaka ya 123 mbali ya kutoka droo ya 2-2 na timu ya Mauritius.
Kenya pia imepanda nafasi moja juu na sasa ipo ya 117 huku ikiwa na rekodi ya kuifunga Shelisheli 2-0 katika mechi yake ya kirafiki.
Mbali na Afrika ya Mashariki, kiujumla kumekuwa na mabadiliko makubwa katika viwango hivyo vya mwezi April.
Miongoni mwa nchi zilizopanda ni Belgium ikiwa ya tatu baada ya kupanda juu nafasi moja kufuatia ushindi wake katika michuano ya Ulaya ya EUFA.
Brazil pia ni miongoni mwa nchi zilizopanda, ikiwa ya ya 5, ikipanda nafasi 1.
Nchi 10 bora katika viwango vya fifa ni
1. Ujerumani
2. Argentina
3. Belgium
4. Colombia
5. Brazil
6. Netherlands
7. Portugal
8. Uruguay
9. Swizerland
10. Uhispania

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages