Bohari ya dawa yaelezea mipango yake ya kazi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Bohari ya dawa yaelezea mipango yake ya kazi

 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa Bohari ya Dawa  (MSD),  Edward Terry (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam mipango ya  MSD na mambo mengine. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka.
 Etty Kusiluka akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Dotto Mwaibale

WASIMAMIZI  wa vituo vya afya, zahanati, hospitali za wilaya, mkoa na hospitali za rufaaa wametakiwa kuwa makini katika kusimamia utoaji wa dawa na vifaa tiba ili kutoa matumizi ya dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha vinatosheleza idadi ya watu katika eneo husika.

Wito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja na shughuli za kanda wa Bohari ya Dawa (MSD),  Edward Terry wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam katika ukumbi wa wa idara habari maelezo.

"Wasimamizi wa vituo vya afya na hospitali huleta maoteo ya dawa na vifaa tiba kulingana na idadi ya watu walionao kwenye maeneo yao na mara nyingi uangalia magonjwa yanayoshambulia zaidi maeneo hayo hivyo hakutakiwi kuwa na uhaba wa dawa endapo usimamizi mzuri utazingatiwa, alisema Terry.

Akitolea mfano wilaya ya Iramba, Igunga, Bariadi, babati , Arumeru na Sumbawanga kutokuwa na tatizo la dawa ambapo hufuata kanuni na sheria za uagizaji wa dawa kutoka bohari ya dawa pamoja na kutumia vyanzo vingine vya mapato kuongezea bajeti inayotolewa na serikali.

Pamoja na hilo  Teryy aliongeza kuwa usimamizi makini wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ndiyo utakaofanya changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye hospitali na vituo kukoma.

"MSD imeboresha huduma na kumpatia mteja taarifa muhuimu zinazomhusu kwa kuziweka wazi taarifa hizo kwenye mtandao ambapo atapata fursa ya kupata taarifa hizo muda wowote.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages