Klabu za Bayern Munich ya Ujerumani na Barcelona ya Hispania zimetinga nusu Fainali katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kushinda mechi zao hapo jana usiku.
Baada ya kuchezea kichapo cha cha bao 3-1 katika mechi ya awali dhidi ya Porto Fc ugenini,hatimaye Bayern Munic waliigeuzia kibao Porto na kuirarua bila huruma bao 6-1 na hivyo kuwa na njia nyeupe ya kutinga nusu Fainali kwa ushindi huo wa jumla ya magoli 7-4.
Nao Barcelona baada ya ushindi wa awali wa bao 3-1 dhidi ya Paris st Germen, mjini Paris ,hapo jana imeendeleza vipigo dhidi ya Wafaransa hao baada ya kuwakandamiza bao 2-0,zilizowekwa kimiani na Mbrazil Neymar katika kipindi cha kwanza.Kwa matokeo hayo Barcelona imefuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-1.
Mechi nyingine za robo fainali zinakamilika hii leo , pale Juventus ya Utaliano itakaposhuka dimbani kuwakabili Monaco ua Ufaransa,huku shughuli nyingine pevu ikitarajiwa kuonekana kwenye dimba la Santiago , pale mabingwa watetezi Real Madrid watakapo wakaribisha mahasimu wao Atletico Madrid.BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)