Ajali nyingine leo TANGA, mabasi mawili na gari ndogo, kuna vifo na majeruhi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ajali nyingine leo TANGA, mabasi mawili na gari ndogo, kuna vifo na majeruhi

IMG-20150409-WA0018
Tangu ilipotokea ajali ya barabarani eneo la Changarawe Iringa ambayo ilitokana na basi la abiria la Kampuni ya Majinjah Express kugongana na lori, stori zikaendelea kuwa nyingi kwenye vyombo vya habari, nyingi zikiandikwa kuhusu vyanzo vya ajali hizo.

Ajali nyingine tena imetokea Tanga leo APRIL 9 2015, taarifa za awali zinasema watu 10 wamefariki na wengine wamepata majeraha kutokana na ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkata, Wilaya ya Handeni Tanga, gari zilizopata ajali hiyo ni basi la NGORIKA, jingine laRATCO pamoja na gari nyingine ndogo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, RPC Juma Ndaki kathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba mwendo kasi umechangia kutokea ajali hiyo.
Hizi ni PICHAZ ambazo zimeenea mitandaoni zikionesha jinsi hali ilivyo eneo la tukio.
IMG-20150409-WA0014IMG-20150409-WA0015
IMG-20150409-WA0016
IMG-20150409-WA0017
IMG-20150409-WA0018
IMG-20150409-WA0013
IMG-20150409-WA0019
#RIP kwa watu wetu waliofariki kwenye ajali hiyo, pole kwa waliopata majeraha pia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages