Pages

Zlatan:Wachezaji wa Chelsea wana 'utoto'

Ibrahimovic akitoka uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu
Wachezaji wa Chelsea walijifanya kama watoto wakati wa tukio lililosababisha mshambuliaji wa Paris St Germain Zlatan Ibrahimovic kupewa kadi nyekundu, mshambuliaji huyo amesema.
Raia huyo wa Sweden alitolewa baada ya kumchezea visivyo kiungo wa kati wa Chelsea Oscar kunako dakika ya 31 lakini PSG ikafanikiwa kuizuia Chelsea na hatimaye kushinda mechi hiyo na kufuzu katika robo fainali.
Nilipopewa kadi nyekundu wachezaji wote wa Chelsea walinikaribia na kunizunguka.
Wachezaji hao wa the Blues pia walimzunguka refa raia wa Uholanzi Bjorn kuipers baada ya kumchezea vibaya Oscar.
Wachezaji wa Chelsea wamzunguka refa baada ya Ibrahimovic Kumchezea visivyo kiungo wa kati wa Chelsea Oscar
''Sijui nikasirike ama kucheka.kwangu mimi wakati nilipoona kadi nyekundu nilijiambia refa huyu hajui anachofanya'' ,mchezaji huo wa PSG alisema.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 33, pia alisema kwamba ''Oscar alijidai kuumia baada ya tukio hilo. Sijui iwapo alikuwa anajifanya ama vipi kitu muhimu ni kwamba tuliibuka washindi''.
Mechi hiyo iliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge ilikamilika ikiwa 2-2 na 3-3 kwa jumla huku PSG ikifuzu kwa kupata mabao mengi ya ugenini.BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)