Pages

Watu 5 wafariki katika shambulizi Baidoa

Alshabaab lavamia mji wa Baidoa
Takriban watu watano wameuawa katika shambulizi katika makao makuu ya serikali ya Somalia mjini Baidoa ambayo ni makao ya rais wa jimbo hilo. Maafisa wa usalama nchini Somalia wanasema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Alshabaab wamepigana na kufanikiwa kuingia katika makao makuu ya utawala wa jimbo hilo katika mji wa kati wa Baidoa . Kulingana na waziri wa usalama katika eneo hilo washambuliaji 3 waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi ya kikosi cha jeshi la Somalia waliuawa baada ya majibizano ya risasi ambayo yaliendelea kwa takriban dakika 20.
Maafisa wawili wa usalama waliuawa huku raia wawili pia wakijeruhiwa.
Ripoti zinaarifu kuwa mashambulizi hayo yalianza kwa mlipuko katika lango la makao hayo kabla milio ya risasi kusikika ndani ya jengo hilo.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa na shirika la umoja wa mataifa zimesema kuwa mashirika mbali mbali yanayotumia jengo hilo hayakulengwa.
Wanajeshi wa Ethiopia walifanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa Alshabaab katika mji wa Baidoa mwaka 2012 baada ya wapiganaji wa kiislamu kuuthibiti mji huo kwa takriban miaka mitatu.BBC swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)