Pages

Watu 12 wamenyongwa Pakistan

Watu 12 wamenyongwa Pakistan
Pakistan imewanyonga watu kumi na wawili kutoka magereza tofauti kote nchini.
Ni idadi kubwa ya mauaji kutekelezwa kwa siku moja tangu serikali iondoe marufuku ya hukumu hiyo kuu mnamo mwezi Desemba.
Pakistan imewanyonga takriban watu arobaini tangu kuanza tena kutumika hukumu hiyo kufuatia shambulio la Taliban dhidi ya shule moja huko Peshawar ambapo watoto wapatao 150 waliuawa.
Serikali imesema kuwa,asilimia kubwa ya waathiriwa ni watu waliopatikana na hatia ya ugaidi mauaji na makosa mengini kama uhaini.
Pakistan imewanyonga takriban watu arobaini tangu kuanza tena kutumika hukumu hiyo
Msemaji wa wizara ya waswala ya ndani ,amesema kuwa takriban watu 8000 wamehukumiwa kinyonga nchini humo.
Aidha wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa asilimia kubwa ya hukumu hizo haziwezithibitishwa iwapo ilitimiza vigezo vya kimataifa vya haki kwa watuhumiwa.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)