Pages

Je furaha ina sauti gani?

Je furaha ina sauti gani?
Je furaha inaweza kuwa na sauti gani ?
Ni swali linaloulizwa na Umoja wa Mataifa ukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya furaha duniani, tarehe 20 Machi.
Kwa maana hiyo Umoja wa Mataifa umezindua kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayoitwa ''#HappySoundsLike''
yaani “Sauti ya Furaha” ukiiomba jamii ya kimataifa kuchagua wimbo bora unaomfanya mtu kufurahi zaidi.
Je furaha ina sauti ?
Katika uzinduzi wa kampeni hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaomba watu wote kuwa na furaha, katika lugha rasmi zote sita za Umoja wa Mataifa.
“Kwenye siku hii, tunatumia lugha ya kimataifa ya muziki kuonyesha mshikamano na mabilioni ya watu duniani wanaoathirika na umaskini,
ukiukwaji wa haki za binadamu, mizozo ya kibinadamu na matokeo ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi”
Aidha amesema kwa upande wake wimbo anoupenda zaidi ni “Signed Sealed Delivered” wa Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, Stevie Wonder.
Je furaha ina sauti gani?
Tungo zitakazochaguliwa na watu zitachezwa katika orodha maalum itakayoandaliwa na kampuni ya muziki ya MixRadio.
Miongoni mwa wasaani watakaoshiriki kwenye maadhimisho hayo mwishoni mwa wiki hii mabalozi wa umoja wa mataifa
Charlize Theron, Lang Lang, Michael Douglas, Midori, Jean-Michel Jarre na Angelique Kidjo pamoja na wasaani maarufu kama David Guetta, Cody Simpson na Pharrell Williams.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)