Mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo Media Krantz Mwantepele akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika kituo cha wazee wasiojiweza Msimbazi kinachosimamiwa na jimbo kuu hapa dar es salaam kanisa la katoliki na kuhudumia wazee wapatao kumi na moja waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu.Timu nzima ya Mwanaharakati Mzalendo Media ilikuja hapa kuwaona wazee hawa na kupata nafasi ya kuwafariji na kutoa baadhi ya misaada ya chakula na nguo za kuwasitiri leo siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015 |
Mdau Marko Mlonganile akipata nafasi ya kumsalimia mmoja ya wazee wanaopatikana katika kituo hiki na kupata nafasi ya kujua baadhi ya changamoto zinazopatikana katika kituo hiki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015 |
Mdau subilaga james akiwa katika taswira na mmoja bibi wanaopatikana katika kituo hiki cha wazee wasiojiweza kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam la kanisa katoliki na kuweza kuhudumia wazee wapatao kumi na moja siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015 |
Baadhi ya wadau toka Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakiongea na mmoja ya wazee aliyelala kitandani ni moja kati ya wanaotunzwa na kituo cha wazee siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015 |
Moja ya nyumba ambayo inatunza wazee wasiojiweza na ni kituo kinachosimamiwa na kanisa katoliki jimbo kuu dar es salaam |
Mahojiano yakiendelea na msimamizi wa kituo hiki sister angelina hapa akieeleza historia fupi ya kituo na jinsi wanavyowahudumia wazee katika kituo hiki |
Mkurungezi wa Mwanaharakati Mzalendo Media Krantz Mwantepele akitoa maelezo kidogo kwa msimamizi wa kituo hiki sister angelina (hayupo pichani ) na wanaosikiliza kwa makini ni wadau Subilaga na Happy |
Wadau wa Mwanaharakati Mzalendo MEDIA wakifurahi jambo na msimamizi wa kituo hiki sister angelina |
Tukikabidhi baadhi ya michango kama mahitaji muhimu ya chakula kwa mismamizi wa kituo cha wazee wasjiojiweza sister angelina anayeshuhudia ni mdau bensoni |
Mmoja wa wazee akiongea jambo mdau Marko mlonganile huku mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo media Krantz Mwantepele akisikiliza kwa makini . |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)