Tona ya Coraltint katika chupa mpya yazinduliwa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Tona ya Coraltint katika chupa mpya yazinduliwa

 Kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali ya Coral paints inaendelea kuonyesha dhamira yake ya dhati kwa wateja wake kwa kuwapatia huduma bora, kuongeza maboresho na ubunifu katika bidhaa zake. Hivi karibuni kampuni hiyo ya rangi imezindua tona mpya chini ya jina la CORALTINT ambayo imeboreshwa na imefanyiwa baadhi ya mabadiliko katika mfuniko wake.

Hatua hiyo ya maendeleo imefikiwa baada ya kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wateja wake katika maeneo mbalimbali. Utafiti uliofanyika pia ulionyesha haja ya kuboresha mfuniko wa tona hiyo ili kukabiliana na harakati, uhifadhi na usafirishaji kwa mtumiaji.

CORALTINT ambayo inapatikana katika chupa ya ujazo wa 50ml imepitia  mabadiliko mbalimbali, hivi hasa kampuni imefanya maboresho muhimu katika ufungaji kwa kuboresha mfuniko, ambao huzuia kuvunjika na kuvuja wakati wa usafirishaji na uhifadhi. Maboresho haya mapya si tu yanafanya tona ya CORALTINT kuaminika zaidi lakini pia yanaipa bidhaa uimara kwa ajili ya miradi mbalimbali. Tona hizi inapatikana katika rangi 12 tofauti zinazowaruhusu watumiaji kuchanganya rangi zaidi ya10,000.

Kulingana na maongezi na Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Coral Paints tona ya CORALTINT si tu hutoa usahihi bora wa rangi lakini pia hutoa muonekano wa hali ya juu na kuifanya  kampuni ya Coral Paints kuwa kampuni pekee ambayo inayoweza kutengeneza  rangi za aina zote kulingana na uhitaji. Bw. Kishan anasema kwamba, "Kutokana na maboresho  haya, wateja wetu wanaweza kuwa na uhakika wa dhamira yetu ya dhati ya kuwapatia huduma bora zaidi. Tunachukua hatua hizi za uboreshaji na ubunifu ili kuendelea kudumisha msimamo wetu kama waanzilishi katika sekta ya rangi nchini Tanzania ".

CORALTINT inatumika katika ujenzi wa majengo ya maofisi, majengo ya makazi na pia katika biashara mbalimbali. Wafanyabiashara nchini kote hutegemea bidhaa kama hizi kila siku ili kukamilisha kazi zao. Hawa watu ni ushahidi tosha wa ufanisi na matumaini juu ya bidhaa kama vile CORALTINT. Mbali na ubora wa rangi unaotolewa na tona pia kuna faida zaidi ya kiuchumi kutokana na bei yake na pia utendaji wake wa kazi ulio bora. Tona hiyo imepokelewa vizuri sana na watumiaji, hasa wale wanaosafiri nazo sehemu mbalimbali.

Tona za Coral Paints zina uwezo wa kuzalisha rangi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya wateja ambayo inadhihirisha faida katika matumizi na bajeti. CORALTINT haibadili uhalisia wa rangi ya kuchanganywa, rangi hubaki na uzito uleule na hivyo basi kumpatia mteja utendaji wa kiwango cha juu.

Siku zote kampuni ya Coral Paints imekuwa mstari wa mbele katika ubunifu. Bidhaa hizo zina sifa za kiwango cha juu katika soko kutokana na utengenezaji imara, bora na zisizo na athari kwa  mazingira.

Kuhusu Coral Paints
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.

Hivi leo, Coral Paints imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini  Tanzania umewezeshwa na  ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini  Uingereza na Pat’s Deco ya  Ufaransa.

Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Coral Paints. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatengenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoedana na thamani- ya -fedha.

Kiufanisi, miundombinu ya Coral Paints inajulikana kwa ubora wake.  Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa.
Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages