Pages

Tanzania yapitisha muswada wa ajira


Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya udhibiti wa ajira za wageni wa mwaka 2014 ,ambapo pamoja na mambo mengine unaainisha vipengele muhimu vya ajira kwa wageni na wazawa.Hata hivyo bunge hilo limesisitiza serikali kupitia taarifa za waomba ajira wageni ili kubaini uwezo kuhusu ajira wazoomba na mienendo yao kijamii.
Sheria hiyo pia inawataka watanzania kuwepo katika ajira zote kutokana na sifa zao.huku wageni wakianishiwa aina ya ajira kulingana na mahitaji ili kuleta ushindani sahihi katika soko la ajira nchini humo.
Sheria hiyo inalenga kuvutia waombaji wenye ujuzi kutoka nje kulingana na mahitaji,huku pia ikitoa fursa kwa wazawa.Akichangia muswada huo kabla ya kupitishwa mbunge wa Karatu Yohana natse anaeleza jinsi wazawa wanavyopaswa kunufaika zaidi
Gaudensia Kabaka ni waziri wa kazi na ajira wa Tanzania na hapa amesema kuwa vibali vya kazi kwa wageni na suala la uraia kwa mjibu wa sheria hiyo ni mambo ambayo hayataenda pamoja,bali kinachotakiwa ni kutumiza masharti yote mawili.
Kupitia muswada huu,bunge limesema kuwa ni moja ya hatua itakayosaidia ajira wa vijana wa Tanzania ambayo baadhi yao wanakosa ajira kutokana na mazingira ya kipaumbele kuwa kwa wageni na si wazawa kama ilivyo katika mataifa mengi duniani ambayo kutoa fursa kwa wenyeji na kisha wageni baadaye.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)