Pages

Al shabaab waua watatu, Kenya

Alshabaab
Maafisa wa polisi nchini Kenya wanasema kuwa takriban watu watatu wameuawa katika mji wa kazkazini wa Wajir, yapata kilomita 100 kutoka mpaka na Somalia.
Watu waliofunika nyuso zao walishambulia duka moja na kufyatua risasi, kulirushia magurunedi kabla ya kulichoma.
Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab limeongeza mashambulizi yake kazkazini mashariki mwa Kenya katika siku za hivi karibuni ,na kufanya mashambulizi mawili katika mji wa Mandera ambao una pakana na Somali.
Kundi hilo linadhibiti eneo kubwa la Somalia la mashambani na limesajili idadi kubwa ya raia Wakenya.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)