Pages

Taharuki yakumba Nigeria kabla ya matokeo

Matokeo ya uchaguzi Nigeria yatarajiwa leo
Uingereza na Marekani zimeelezea masikitiko yao kuwa kumekuwa na wizi wa kura, katika uchaguzi mkuu uliomalizika siku ya Jumamosi Nchini Nigeria.
Mwaandishi wa habari wa BBC wa maswala ya Afrika aliyeko Nigeria anasema kuwa hali ni ya wasiwasi katika mji mkuu Abuja.
Katika taarifa ya pamoja, yanasema kuwa wameona dalili za kutiliwa shaka kuwa kumekuwa na uingiliaji wa kisiasa na utaratibu mzima wa uchaguzi mkuu kuvurugwa.
Aidha wachunguzi wa mataifa mengi waliokuwa wakichunguza shughuli za upigaji kura hapo siku ya Jumamosi, wamesifia uchaguzi huo.
Tume ya uchaguzi mkuu Nchini humo inasema kuwa kuna uwezekano kuwa mshindi wa uchaguzi huyo atajulikana hatimaye leo Jumatatu, na mshindi kutangazwa kesho Jumanne.
Kinyang'anyiro kikuu ni kati ya Rais wa sasa Goodluuck Jonathan na aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Mohamadu Buhari.
Mawakala wa wagombea viti wakipiga msasa matokeo mjini Lagos
Ni ushindani mkali zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi miaka 16 iliyopita.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.
Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega.
"Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011.
Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana.
Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi."
Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi.
Wasimamizi wa uchaguzi nchini Nigeria wakihesabu kura
"Tunaamini tumefanya vizuri kabisa.
Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo.
Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha.
Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi,
ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega.
Mama akipiga kura nchini Nigeria
Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani.
Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo.
Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais,
Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC
na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)