Kutokana na mpango mkakati wa
serikali wa mwaka 2012 mpaka 2017 ambao unalenga upanuzi wa makazi katika mikoa
mbalimbali, kumekuwa na ongezeko kubwa la
majengo ya makazi, majengo ya ofisi na
majengo ya masoko ambayo yameonekana
kuwa na manufaa na mchango mkubwa katika sekta mbalimbali na viwanda
nchini Tanzania. Mpango huu wa upanuzi umejenga mahitaji kwa vifaa vya ujenzi
ambapo kwa upande mwingine imeonekana kuwa ni faida kwa wauzaji ambapo wauzaji
wengi wamekuwa na jitihada katika
kuongeza kasi na namna ya uendeshaji
na utoaji wao wa huduma ili kukabiliana na mahitaji mapya.
Kama ilivyo kwa saruji na vyuma,
rangi pia imekuwa ni bidhaa kubwa na moja ambayo imekuwa ikihitajika sana
kutokana na maendeleo ya miundombinu. Maendeleo haya ya kasi yamesababisha
mabadiliko kwenye sekta ya rangi pia ili kukabiliana na mahitaji
yanayojitokeza. Hii imesababisha kuanzishwa kwa teknolojia mpya, bidhaa na njia
za kibunifu ili kukidhi mahitaji muhimu kwa ajili ya ubora unaoitajika.
Katika ulimwengu huu wa teknolojia soko la rangi pia limekuwa
likibadilika kuendana na maendeleo yaliyopo. Kumekuwapo na utumiaji wa mashine zinazotumia
kompyuta ambazo zimepunguza muda
ufanyaji kazi na kuwa msaada mkubwa sana wasanifu na makandarasi wakiwa katika
ujenzi.
Haya yameelezwa na Bw. Kishan
Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd. Moja ya kampuni kubwa
nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Anasema kuwa
"iwe kwa ajili ya nyumba, biashara au viwanda soko
la rangi nchini lipo katika hatua kubwa kutokana na maendeleo ambayo yanatokea
hivi sasa. Sekta hii inaweza kusimama kutokana na mchango mkubwa inayoleta
katika uchumi wa nchi"
Kampuni ya Insignia ni mfano wa
kampuni ndogo ambayo imepitia mitihani mingi
na hatimaye imekuwa kiongozi na kuleta mabadiliko katika soko la rangi nchini. Tangu kuanzishwa kwake mkoani
Moshi (Kilimanjaro) kampuni hii sasa imeonyesha matunda yake. Bw Kishan pia ametoa
maoni kwamba makampuni ya kisasa ya rangi kama vile Insignia hayana budi
kudumisha ujasiriamali wake ambao umekuwa kama uti wa mgongo wa ukuaji wake. Na
katika maendeleo hayo vilevile anatoa
wito wa kuwa na "nia ya dhati
na ubunifu ambao utasaidia katika ukuaji zaidi wa soko hilo. "
Kuanzia kwenye majengo ya makazi
na majengo ya viwanda rangi inahitajika sana katika ujenzi wake. Miongoni mwa
huduma mbalimbali zinazotolewa na Insignia ni pamoja na 'THE ART', inayotumika kulingana
na mahitaji ya mteja.
Maendeleo ya makampuni kama vile
Insignia kutoka biashara ndogo na kuwa kampuni kubwa ni ushahidi tosha katika
soko la rangi kama moja ya sekta inayoshirikiana na sekta nyingine katika kuchagiza uso wa miundombinu ya nchi yetu.
Kuhusu Insignia
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia
kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta
ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa
sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.
Hivi leo, Insignia imefikia moja
ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika
utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango
vya hali ya juu nchini Tanzania
umewezeshwa na ushirikiano na makampuni
makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal
iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco
ya Ufaransa.
Bidhaa mbili za Coral na Galaxy,
zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza
rangi na bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia
ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa
sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatengenezwa kiufundi, inatumia ujuzi,
pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa
kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini
Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora
inayoedana na thamani- ya -fedha.
Kiufanisi, miundombinu ya Insignia
inajulikana kwa ubora wake. Viwanda vyake
vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya
kimataifa.
Kampuni hii ina viwanda jijini
Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi,
Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana
wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa
nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)