Simba yaendeleza ubabe kwa Yanga - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

demo-image

Simba yaendeleza ubabe kwa Yanga

MMGL0019
Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (mwenye miwani) akiongozana na wadau mbali mbali wa IMETOSHA MOVMENT pamoja na wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakiingia Uwanjani,ikiwa ni katika muendelezo wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino yaliyobeba ujumbe wa IMETOSHA.Picha kwa Hisani ya Othman Michuzi wa Michuzi Media
MMGL0036
Sehemu ya Wachezaji timu za Simba na Yanga wakiwa wamevalia fulana zenye ujumbe wa IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO,wakati wakiingia uwanjani.
MMGL0056
MMGL0092
Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa tatu kushoto) akizungumza machache juu kampeni yake ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino iliyobeba ujumbe wa IMETOSHA MAUAJI YA ALBILO,kabla ya kuanza kwa kipute cha Simba na Yanga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
MMGL0115
Kikosi cha Simba.
MMGL0123
Kikosi cha Yanga.
MMGL0169
 Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan akiwania mpira na Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Simba imeshinda bao 1 - 0 lililotiwa kimiani  kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
MMGL0172
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
MMGL0229
 Nyanda nambari moja wa timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwa ametulia langoni kwake tayari kwa kuzuia shuti lililopigwa na Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
MMGL0260
Wakati mtanage ukiendelea,ghafla likatokea zogo baina ya Nahodha wa Timu ya Yanga na Kiungo wa Simba,Abdi Banda na mambo yalikuwa hivi.
MMGL0320.
"Beki hasififiiiii lakini hapa anastahili sifa....",Beki wa Simba,Juuko Murshid akiruka juu kuondoa mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake,mbele ya Washambuliaji wa Yanga.
MMGL0349
Kipa wa Yanga,Ally Mustafa "Bartez" akiwa ameruka juu kuondoa hatari langoni kwake.
MMGL0352
Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Simba.
MMGL0356
Beki wa Simba,Kessy Ramadhan akimzungusha mshambuliaji wa Yanga.
MMGL0364
Anacheza paleeeee Ivo Mapunda.
MMGL0372
Haya nendeni kuleeeeee...... 
MMGL0381
Wee kipa hili Taulo lako silitaki hapa,naliweka huku nje.
MMGL0397
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akiachia nduki kali ambalo hata halikuzaa matunda.
MMGL0437
Mashabiki wa Yanga wakijifariji.
MMGL0451
Washabiki wa Simba wakiwabeza wenzao wa Yanga.
MMGL0489
Wadau wa IMETOSHA wakiendelea kuwakilisha uwanjani.
MMGL0520
MMGL0506
Umati wa Washabiki wa Timu ya Simba ukiwa umefurika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam kuipa sapoti timu yao ambayo haikuwaangusha leo,baada ya kuwatandika bao 1 - 0 watani zao wa jadi Yanga,lililotiwa kimiani  kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
MMGL0537
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika kabisa.
MMGL0542
Hatari lakongoni mwa timu ya Simbaaaaa....
MMGL0547
Kadi Nyekunduuuuu kwa Mchezaji wa Yanga,Haroun Niyonzimaaaaa.... baada ya kupiga mpira ulioingia wavuni baada ya refa kupiga filimbi kuwa ni faulo.
MMGL0553
Niyonzima anamzonga Mwamuziii
MMGL0557
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akizungumza na Mwamuzi juu ya Kadi aliyopewa Niyonzima.
MMGL0625
Ukiangalia vyema utabaini kitu.
MMGL0638

MMGL0683

MMGL0685

MMGL0721

MMGL0726
Furaha ya ushindi.
MMGL0772

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages