Ruhusuni wanaume waingine wadi za leba - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ruhusuni wanaume waingine wadi za leba

DSC_0036
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha maelezo kazi zinazofanywa na taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15. Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na mama.

Alisema wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.

Naibu waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa wiki.
Alisema yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume kukalishwa chini kuelekezwa.
DSC_0069
Muuguzi wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Aidha ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.
Alisema pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi wa watoto njiti.
Alisema kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.
Awali wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto njiti waweze kuendelea kuishi.
DSC_0194
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Wakati huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema kwamba yeye alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 alisema zaidi ya watoto 200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.
Alisema wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka hospitalini.
Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa.
Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
DSC_0112
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akielezea makuzi yake baada ya kuzaliwa njiti wa uzito wa kilio 1.2 na kuona kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.
DSC_0158
DSC_0171
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimpongeza Balozi Mwanaidi Sinare kwa risala nzuri aliyoitoa wakati wa sherehe za uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency mwishoni mwa wiki jijini Dar. Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
DSC_0274
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza na kumpongeza Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
DSC_0204
Meza kuu wakijianda kuelekea sehemu maalum ya kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
DSC_0218
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel na mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba kwa pamoja wakikata utepe kuzindua taasisi yao huku Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Balozi Mwanaidi Sinare wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0220
Sasa imezinduliwa rasmi.
DSC_0222
DSC_0228
Balozi Mwanaidi Sinare (kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel kwenye uzinduzi huo.
DSC_0294
Sehemu ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
DSC_0305
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0240
Meza kuu kwa pamoja wakikata cake maalum wakati wa uzinduzi huo.
DSC_0250
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi.
DSC_0252
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Balozi Mwanaidi Sinare.
DSC_0254
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha cake Muuguzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda (kushoto).
DSC_0256
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba.
DSC_0258
DSC_0261
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha kipande cha cake mama yake mzazi Celina Mollel.
DSC_0048
Rachel Temu, William Malecela pamoja na mdau wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel.
DSC_0053
DSC_0040
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo (kulia) Mdau wa Doris Mollel Foundation, Suleiman Saleh pamoja mgeni mwalikwa.
DSC_0268
Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi (kulia).
DSC_0025
Mtangazaji wa kituo cha Channel Ten na Magic FM, Salma Msangi na rafiki yake wakati wa uzinduzi huo.
DSC_0080
Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo Leo, Juma Pinto (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Benny Kisaka (wa pili kulia) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo.
DSC_0316
Mama mzazi wa Doris Mollel , Bi. Celina Mollel (kushoto) katika picha ya pamoja na wadau waliojitokeza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Ramesh Patel.
DSC_0026
Mjasiriamali Maznat Yusuph Sinare (aliyesimama katikati) akiteta jambo na Balozi Mwanaidi Sinare (kulia) kwenye sherehe fupi za uzinduzi wa Doris Mollel Foundation.
DSC_0021
Balozi Mwanaidi Sinare akisalimiana na Mh. Iddi Simba (aliyeipa mgongo kamera yetu) Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
DSC_0321
Mwenyekiti wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kushoto) Balozi Mwanaidi Sinare pamoja na mshirika mwenza wa taasisi ya Doris Mollel, Heena Mujtaba.
DSC_0327
Pichani juu na chini ni Doris Mollel na familia yake akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria uzinduzi wa taasisi yake.
DSC_0331
DSC_0336
DSC_0341
Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Rafiki wa Doris Mollel ambaye ni Mlemavu Sophia.
DSC_0346
Kutoka kushoto ni Msanii wa filamu nchini, Sinta, Hoyce Temu pamoja na Rachel Temu wakipiga picha kumbukumbu mara baada ya uzinduzi huo kufikia tamati.
DSC_0350
Doris Mollel na Sintah.
DSC_0359
Mdau Chiku Lweno (kulia) akipozi na Doris Mollel pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages