Pages

Real Madrid yachapwa na Barcelona 2 - 1

Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga goli la pili kwa upande wa Barcelona
Real Madrid ya Hispania jana ilidondokea pua katika mechi ya kukata na shoka baina yake na mahasimu wao Barcelona baada ya kukubali kichapo cha magoli 2 -1.
Katika mechi hiyo maarufu kama El Clasico ambayo hushudiwa na mamilioni ya wapenzi soka duniani kote Barcelona waliikimbiza mchakamcha Real Madrid na kuifanya ihemee juu juu.
Jeremy Mathieu ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua kitabu cha magoli cha Barcelona pale alipoandika bao la kwanza katika dakika ya 19 huku wakiwa bado wameduwaa mshambuliaji wa zamani wa Livepool Luis Suarez akapigilia msumari wa moto kwenye kidonda pale alipotikisa wavu wa Real Madrid katika dakika ya 56 na kuandika bao la pili.
Goli pekee la kufutia machozi la Real Madrid lilifungwa Christiano Ronaldo katika dakika ya 31.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)