Naye Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mbunguni amewaambia wananchi katika mkutano huo amemshutumu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kwa kutosikiliza ushauri alioutoa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa wilayani Loliondo na Ngorongoro kwa mawaziri ambao wizara zao zinahusika moja kwa moja katika maamuzi na kushughulikia matatizo ya migogoro ya Ardhi mkoani Arusha ambapo kumekuwa na migogoro karibu wilaya zote, kati ya mbuga za wanyama na vijiji ama kati ya vijiji na vijiji.
Nape amesema wakati waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiitikia na kupokea ushauri huo na kuhamishia shughuli zake mkoani Arusha ambapo kwa sasa yuko mkoani humo akikutana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi ili kutatua migogoro hiyo, Nyalandu amekaa kimya anaendelea na mambo yake.
CCM ndiyo yenye mkataba na wananchi kwani ndiyo iliyoomba kura kwa wananchi na Mh Waziri Nyalandu ana mkataba na CCM ambayo imempa kazi ili afanye kazi na kutatua matatizo ya wananchi, CCM haiwezi kukubali mambo yaiharibike kwa watendaji wa serikali kutowajibika kwa wananchi kwani ndiyo itakayoadhibiwa na wananchi wakati wa uchaguzi ujao, "Hivyo Nyalandu anatakiwa kufanya kazi ambayo CCM imempa na si kutafuta watu wa kumtetea si sawa" Amesema Nape Nnauye.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MERU-ARUSHA





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)