Pages

News Alert: Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kuaga mwili wa Kapteni John Komba

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa marehemu Salome Komba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete (katikati) akijadiliana jango na Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Wengine pichani toka kushoto ni Rais Mstaafu,Mh. Ali Hassan Mwinyi,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete pamoja na Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee leo.Picha kwa Hisani ya Michuzi Media. PICHA ZAIDI ZITAWAJIA HIVI PUNDE

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)