Pages

Mrisho Ngassa aweka ngumu kusaini mkataba mpya katika klabu ya yanga

Mrisho Ngassa amegoma kusaini mkataba mpya na Yanga mpaka uongozi utakampomlipa deni lake la Sh45 milioni, akidai kwamba uongozi wa Yanga ulimuhadaa akope fedha zake benki ya CRDB ili ailipe Simba kwa kile walichomuadi kumlipia deni hilo. 

"Yanga wasipotoshe ukweli...wao waliniambia nikope fedha, watalipa. 
Matokeo yake wananikata mshahara wangu wote, nimegoma kusaini ndiyo! Mpaka wanilipe deni langu Sh45 milioni wakishanilipa nitakubali kukaa mezani tujadili mkataba mpya."alisema mshambuliaji huyo,  Ngassa, ambaye pia amewahi kuchezea Kagera Sugar, Azam , na Simba ambaye pia amefunga mabao 28 Taifa Stars katika mechi 80 alizoichezea, aliangukia kwenye deni hilo kubwa kwa hadhi ya wachezaji wa ndani ya Tanzania baada ya kuamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuilipa Simba Sh milioni 30 na penalti ya asilimia 50 (Sh. milioni 15) baada ya kupatikana na kosa la kusaini mikataba ya kuzitumikia  Simba na Yanga msimu uliopita. 

Ngasa alilazimika kukopa pesa CRDB kwa udhamini wa klabu hiyo ya Jangwani, na mara kwa mara amekuwa akilalamikia kitendo cha hivi karibuni klabu hiyo kumkata mshahara wake wote bila kumpa hata shilingi. 
Kauli ya Ngassa amekuja kukiwa na taarifa kuwa amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo hadi hapo uongozi umlipe dola 100,000 sawa na Sh180 milioni kama fedha za usajili na kumpatia mshahara wa dola 5,000 sawa na Sh milioni 9 kwa mwezi. 

"Viongozi wanafanya juhudi za kumuomba apunguze, hiyo hela ni nyingi sana klabu haiwezi kumpatia lakini mpaka sasa Ngassa ameweka ngumu na uongozi umeshaanza kukata tamaa iwapo atashikilia msimamo wake basi itamuachie aende timu anayopenda.

 Akizungumzia suala hilo katibu mkuu wa Yanga Jonas Tibohora alisema "Tunasikia tu Ngassa anaondoka lakini mwenyewe ukimuliza anakataa, hakuna klabu yoyote iliyowasiliana na sisi kwa ajili ya suala hilo." 
Ofisa uhusiano wa Yanga Jerry Muro aliwahi kukaririwa akisema kuwa Ngassa hakuna fedha anazodai klabu hiyo na kwamba deni lililopo ni lake Ngassa na benki ya CRBD.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)