Pages

Heriya kuzaliwa mama mzazi wa blogger Father Kidevu

TAREHE ya leo ni ndio aliyo zaliwa Mama mzazi wa Blogger na Mpigapicha nguli Tanzania, Mroki Mroki, Bi. Mary O.Nathan  (pichani) wa Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye leo anatimiza miaka 63 tangu kuzaliwa kwake tarehe kama ya leo. 


Kipekee anamshukuru Mungu kwa kumjalia umri huo alionao hivi sasa. Anawashukuru wote ambao wamechangia yeye kuishi vyema. Anaishukuru sana Familia yake yote kwa umoja na upendo walio nao jambo mabalo anasema linamfanya aishi kwa furaha na amani. 

Aidha watoto wake wote wanampa Pongezi za dhati na Kumuombea Mungu amjalie zaidi Afya njema, akimpa zawadi ya Hekima na Busara katika kipindi hiki cha maisha yake ya utu uzima ambao Busara yake na Hekima vinahitajika sana ndani ya Familia yake na Jamii kwa ujumla.

Wajukuu zako na Vitukuu wako pia wanakusalimia sana na wanakuimbia kale kawimbo ka Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!!

Happy Birthday Bibi!!! Dear Bibi Happy birthday to youuuuuuuu!!!!

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze ,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakutakia heri na fanaka.

HAPPY BIRTHDAY MAMA TUNAKUPENDA SANA NA TUNAJIVUNIA KUWA NA MAMA WA NAMNA YAKO, MUNGU AKUJALIE HEKIMA NA BUSARA ZAIDI KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO. 

BY: FAMILIA YAKO.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)