Mrembo Miss Tanzania aongoza wakazi wa dar katika zoezi la uchangiaji damu - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mrembo Miss Tanzania aongoza wakazi wa dar katika zoezi la uchangiaji damu

Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la
uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake
Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto  Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la  uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo. 


Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani,mrembo Doris Mollel
ambaye ni Miss Tanzania namba tatu kwa mwaka 2014 ameongoza mamia ya  watanzania katika zoezi la kizalendo la kuhamasisha kuchangia damu kwa  watanzania kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali,zoezi ambalo limefanyika  jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. 


Zoezi hilo ambalo lilikuwa  linaongozwa na mpango wa taifa wa damu salama kwa udhamini wa kampuni ya METL lilikuwa na lengo la kupata damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwani matatizo ya damu katika hospitali za Tanzania  yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,jambo lililompelekea mrembo huyo  kuamua kujitoa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi  hilo. 

Zoezi hilo lilifanyika Machi 8 mwaka huu katika maeneo ya Buguruni  Chama kwa muda wa siku nzima,ambapo jumla ya uniti 65 za damu  zimepatikana kiwango ambacho kimetajwa kuwa kinatia matumaini kwa mrembo huyo kufanikiwa katika kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi. 

Akizungumza na wanahabari kuhusu kitu kilichomsukuma  kuendesha zoezi hilo,Doris alisema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya  kugundua kuwa wakina mama wengi pamoja na watoto hufariki dunia wakati wa
kujifungua kutokana na kukosa damu ya kuongezewa,jambo ambalo amesema ni lazima watanzania kuungana kwa pamoja kutafuta damu ya kutosha katika  kila hospitali ili kuiondoa hali hiyo ambayo inaweka hatarini maisha ya  mama na mtoto wa kitanzania. 


Amesema kuwa swala la  kujitolea damu ni swala la kizalendo zaidi na moyo wa kujitoa kwa kuwa  kila mtanzania anaweza kuwa na uhitaji wa damu muda wowote hivyo ni  lazima watanzania wawe na utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara  kwani itasaidia endepo kutatokea uhitaji wa damu katika mahospitali  yetu. 

Aidha amewataka watanzania wengine ambao wanauwezo  wa kuhamasisha watu wengine kuchangia damu wafanye hivyo kwani kuna  uhitaji mkubwa sana wa damu katika mahospitali ya kitanzania na kufanya  hivyo ni kuokoa maisha ya watanzania wengi wenye uhitaji wa damu hiyo. 

Doris Mollel alijizolea umaarufu mwaka 2014 baada ya kufanikiwa kushika
nafasi ya tatu katika shindano la Miss Tanzania mwaka huo ambapo  aliwashinda warembo wengine waliokuwa wanawania taji hilo.

 Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick,Bi Mariam Meck Sadick akiungana na wananzania wengine kwenye zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mrembo Doris Mollel.
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishiliki zoezi la uchangiaji damu
katika kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni
Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mpiga
Picha wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,John Dande akipima uzito
tayari kwa kushiriki zoezi la uchangiaji damu,ikiwa ni sehemu kuunga
mkono sherehe za Siku ya wanawake Duniani.zoezi hilo lilifanyika
Buguruni Chama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Picha na John Dande.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages