Pages

Majambazi yapora silaha na kutumia kuiba kwenye duka la vinywaji leo Mikocheni kwa mwalimu

Raia waliokuwepo eneo la tukio wakishangaa.Duka la vinywaji lililoibiwa.Sehemu ambayo majambazi wameiba bunduki aina ya Shot Gun.Askari akiwa ndani ya duka la vinywaji akifanya mahojiano na wahusika.
VITENDO vya ujambazi vinazidi kushika kasi kwenye jiji la Dar es Salaam, ambapo tukio lingine limetokea leo mishale ya saa kumi jioni maeneo ya Mikocheni Kwa-Mwalimu Nyerere baada ya watu wanne kutinga eneo hilo wakiwa na pikipiki na kumpora mlinzi silaha aina ya Shot Gun aliyekuwa akilinda kwenye ATM ya CRDB. 
Majambazi hao waliitumia bunduki hiyo kwa kuvamia duka la vinywaji lililokuwa jirani na kuiba kiasi kikubwa cha pesa japo hakikuweza kufahamika kwa wakati huo.
Mtandao huu ulifanya juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Kinondoni, Camillus Wambura ili kupata undani wa tukio hilo na kiasi cha fedha kilichoibiwa ila simu yake ya mkononi ilipokelewa na msaidizi wake aliyedai kuwa kamanda alikuwa katika kikao.
(HABARI/PICHA: MAYASA MARIWATA NA SHANI RAMADHANI/GPL)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)