Pages

Dr Slaa atinga Kituo Cha Polisi cha kati kwaajili ya kueleza tuhuma za kutaka kujaribiwa kuuwawa na mlinzi wake

Akihojiwa na Wanahabari.    ..Slaa(kulia), akitoka katika lango kuu la kituo cha Polisi akiwa na viongozi wengine wa chama hicho.
Waandishi wa habari (kulia) wakimsubiri Slaa nje.Gari la Dr. Slaa likiwa limepaki nje ya Kituo cha Polisi Central.
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dr. Willbroad Slaa, ameripoti katika Kituo cha Polisi Central kilichopo Posta jijini Dar kuhusiana na sakata zima la mlinzi wake anayetuhumiwa kutaka kumuua.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo, Slaa alisema yeye hakuitwa na Jeshi la Polisi kujielezea bali kutokana na maneno yanavyozidi kusambaa na kuwasilishwa ndivyo sivyo ameona aende kueleza ukweli ulivyo.
Alisema kuwa, kwa mujibu wa chama chake, ameona ni vyema kwenda kulieleza Jeshi la Polisi kuhusiana na ishu nzima inayomkabili mlinzi wake, ambapo alikutana na Kamanda wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleimani Kova na kumueleza kila kitu kwa kuandika karatasi tisa (9) zenye maelezo yake, hivyo zoezi zima la kutoa taarifa kuhusiana na alichoandika ameliachia Jeshi la Polisi baada ya wao kufanya kazi yao ya Uchunguzi.
“Ndugu zangu wanahabari sijaitwa hapa kwa ajili ya mahojiano kama taarifa zinavyozaga lakini kutokana na uongozi nilionao nimeona ni vyema suala hili nilifikishe Polisi, na katika maelezo yangu nimeweza kuandika zaidi ya karatasi tisa (9) zenye ukweli mtupu, hivyo nimelikabidhi Jeshi la Polisi na baada ya wao kufanya uchunguzi litatoa taarifa kamili juu ya kile nilicho kiandika,’’ alisema Dr. Slaa.
                         (PICHA/STORI NA DENIS MTIMA/GPL)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)