Dk.Anand Khakhar mshauri wa upasuaji wa Ini katika hospitali ya Apollo.
Ini pamoja na kuwa chombo kikubwa katika mwili wa binadamu pia ni kiungo
muhimu kwa ajili ya kazi za kimwili kwa maana iyo ni vigumu kwa mtu kuishi bila
Ini. Kutokana na maendeleo katika mbinu za kisasa za upasuaji, kwa sasa
upasuaji unafanyika kwa watu wengi zaidi kuliko miaka ya nyuma kwa kuwa watu
wengi wako tayari kufanyiwa upasuaji
kutokana na kuboreshwa kwa viwango vya mafanikio ya upasuaji. Maradhi
sugu ya Ini yanaweza kusababisha mtu kuhitaji upandikizaji ambao kwa kawaida
unapendekezwa kwa watu walio kwenye hatua ya mwisho za magonjwa ya Ini (ESLD –
End Stage Liver Diseases).
Ini linawajibika kwa kazi kadhaa muhimu za mwili kama vile kubadilisha
chakula kuwa nishati na kusafisha damu kutokana na sumu na madawa ya kulevya.
Kiungo hiki pia kina uwezo mkubwa wa kubeba damu, kwa wakati mmoja ina uwezo wa
kua na karibu asilimia 13 ya damu ya mwili.
Miongoni mwa magonjwa yanayoathiri Ini ni pamoja na homa ya manjano,
saratani, ugonjwa sugu wa mirija ya Ini (cirrhosis) ambao pia ni mchangiaji
mkuu katika kusababisha mtu kuitaji upandikizaji. Haya pia ni miongoni mwa orodha
ya magonjwa sugu ambayo hatua kwa hatua yanakuwa mzigo kwa kiwango cha
kimataifa. Kulingana na shirika la afya duniani inakadiriwa 46% ya magonjwa na
59% ya vifo ni matokeo ya maradhi sugu. Katika mtazamo mwingine inasemekana
kuwa watu milioni 35 wanaokufa kila mwaka ni waathirika wa ugonjwa sugu na
takwimu zinaongezeka.
Kimataifa magonjwa ya Ini yanashika nafasi ya tano kwakusababisha vifo
yakiwa nyuma ya kansa na magonjwa ya moyo, kiharusi na ugonjwa wa kifua. Hata
hivyo watafiti wanasema kuwa tofauti na magonjwa mengine kiwango cha vifo vya
magonjwa ya ini yanaongezeko badala ya kupungua. Kwa Tanzania miongoni mwa magonjwa
ya kuambukiza zaidi ni Homa ya Manjano A na Homa ya Manjano E (Hepatitis A and
Hepatitis E). Yote ni magonjwa yanaosababishwa na virusi huenea kwa maji machafu au
chakula na kuingilia utendaji kazi wa ini. Virusi pia ni mtesaji mkuu kwa
kiwango cha kimataifa, katika yote Homa sugu ya manjano ni mchangiaji vifo
1.3million duniani kote takwimu ambazo zinalinganishwa na mzigo wa TB, VVU /
UKIMWI na malaria.
Upandikizaji wa Ini unahusisha kubadilisha Ini lenye ugonjwa na Ini zima
au sehemu ya Ini zima kutoka kwa mtu mwingine. Kwa sasa hakuna mashine ambayo
inaweza kuiga kazi ya Ini utaratibu huu hatari unafanywa tu kama kuna ukosefu
wa tiba nyingine. Pamoja na kiwango cha mafanikio yake ya hivi karibuni
utaratibu huu una uwezekano wa kusababisha kifo kutokana na matatizo wakati na
baada ya tukio hilo.
Dkt. Anand Khakhar Mshauri Mwandamizi wa upandikizaji na Upasuaji wa Ini na
Mkurugenzi Programu ya Kupandikiza Ini katika Kituo cha Magonjwa ya Ini na
Upandikizaji, Hospitali za Apollo, Chennai, India anasema kwamba "kuna mbinu 3 za
upandikizaji Ini: upandikizaji kutoka kwa maiti, upandikizaji kutoka kwa mtu
hai na upandikizaji aina ya tatu ni upandikizaji wa sehemu ya ini ambao haitumiki mara kwa mara. Katika
upandikizaji kutoka kwa maiti Ini la mtoaji linachukuliwa kutoka kwa mtu ambaye
amegundulika amekufa, ambaye familia yake imejitolea kuchangia ogani kwa ajili
ya upandikizaji. Watu ambao wanatakiwa kufanyiwa upandikizaji kutoka kwa maiti
husubiri katika orodha ya taasisi/kanda mpaka wapatikane wafadhili
wanaofaa."
"Kupandikiza kutoka kwa mtoaji Hai
inahusisha mwanafamilia mwenye afya, kwa kawaida mzazi, ndugu, au mtoto, au mtu
wa karibu kihisia, kama vile mke, kujitolea kuchangia sehemu ya Ini kwa ajili
ya upandikizaji. Mfadhili anatathminiwa kwa makini na timu inahakikisha hakuna
madhara yanayoweza kutokea kwa mfadhili au mpokeaji.”
"Upandikizaji wa msaada unahusisha
sehemu ya ini ya mtoaji mtu mzima mwenye afya (hai au maiti) kupandikizwa kwa
mpokeaji. Ini la mgonjwa linabaki kama lilivyo mpaka kipande kisaidizi
kinapoanza kufanya kazi. Ini lenye ugonjwa linaweza sasa kuondolewa."
Mapema mwezi huu timu ya
madaktari kutoka Hospitali ya Apollo , Kituo cha Magonjwa ya Ini na
Upandikizaji (CLDT) wakiongozwa na Dkt.
Anand Khakhar na Dr Anil Vaidya wamefanikiwa kufanya “Multi-Visceral” ya
pili kwa wagonjwa wengi kwa hisani ya maiti ya mtu. Kupandikiza Ini ambako ni
kawaida hufanyika kwa mpokeaji mmoja, lakini mara kadhaa hugawanywa kusaidia
mtu mzima na mtoto, katika tukio hili pia liligawanyika kwa watu wazima wawili,
ushirikiano ambayo ni mara chache kufaniikisha. Kwa kufanya hivyo hospitali hii
inakuwa ya kwanza kufanya operesheni hiyo nchini India kwa mtu anayeteseka kwa
tumbo kushindwa kufanya kazi vizuri tangu utotoni. Kesi hii pia ilikuwa ya
kwanza ambapo ukuta wa tumbo ulipandikizwa juu na katika matumbo ili kuondoa
tofauti kati ya mtoaji na mpokeaji wa matumbo.
Kuhusu Kitengo cha upandikizaji wa Ini katika Hospitali za Apollo.
Huduma
upandikizaji wa Ini katika Hosipitali ya Apollo inalenga kutoa huduma kwa
ufanisi kwa wagonjwa wa ini. Upandikizaji Ini wa mafanikio, unaotolewa katika
hospitali za Apollo ni wa uhakika.
Hospitali za
Apollo zina Kitengo kikubwa sana cha upandikizaji wa
Ini nchini India chenye
mpango madhubuti wa uhifadhi na upatikanaji wa Ini kwa ajili ya upandikizaji
Hospitali za Apollo
zilizopo Delhi, Chennai, Hyderabad, Kolkata, Ahmedabad na Bangalore hutoa upasuaji na upandikizaji wa ini
na ndivyo vinavyofanya kuwa mtandao mkubwa wa upandikizaji wa ini nchini India.
Hospitali ya
Apollo ya Indraprastha, iliyopo mjini Delhi imefanikiwa kufanya upandikizaji wa
ini kwa wagonjwa 200 kutoka Pakistan Novemba 2011. Kwa kiwango cha zaidi ya asilimia
90% kupitia mafanikio yake, Hospitali ya
Apollo ya Indraprastha imejijengea historia kubwa katika ulimwengu wa tiba kwa
kuwa hospitali ya kwanza nchini India
kutibu wagonjwa 200 kutoka nchi hiyo moja.
Kwa mafanikio
ya zaidi ya asilimia 90% upandikizaji wa Ini zaidi ya 500 umefanyika.
Hospitali za Apollo
hufanya zaidi ya upandikizaji 537 wa ini, figo na moyo katika siku 238 na
kufanya hospitali hiyo kuwa ya pili duniani katika kufanya upandikizaji wa
idadi kubwa kwa kipindi kifupi.
Chini ya
miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, timu katika Idara ya ugonjwa wa ini na
upandikizaji ya hospitali ya Apollo, imefanya upandikizaji
wa ini zaidi ya 100 Juni 2011, na hivyo kujichukulia umaarufu mkubwa Chennai.
Upandikizaji
wa ini wa mafanikio kwa watoto na watu wazima kwa mara ya kwanza ulifanywa
katika Hospitali ya Apollo ya Indraprastha, New Delhi mwaka 1998. Tangu wakati
huo, kumekuwa hakuna kuangalia nyuma, na leo ni hospitali kubwa inayoongoza
katika upandikizajia wa ini Asia ya Kusini. Baadhi ya mafanikio ya kihistoria yake
ni:
- Upandikizaji wa mara ya kwanza
wa ini kwa watoto -1998
- Upandikizaji wa mara ya kwanza
wa ini kutoka kwa mtu aliyekufa -1998
- Upandikizaji wa mara ya kwanza
wa ini na figo -1999
- Upandikizaji wa mara ya kwanza
wa ini kwa watoto kutoka kwa mfadhili aliye hai -1999
- Upandikizaji wa mara ya kwanza
wa ini kwa mtu aliyekwisha pandikizwa tayari -2002
- Upandikizaji wa mara ya Kwanza
wa ini kwa mtoto kutoka kwa mtu aliyekufa -2007
- Upandikizaji mdogo wa ini kufanyika nchini India -2008
- Upandikizaji wa Ini na figo
zaidi ya 250 ndani ya mwaka ulifanyika 2009.
- Timu ya Upandikizaji wa Ini katika
Hospitali ya Apollo, Chennai imefanya upandikizaji wa Ini zaidi ya 200. Na hivi sasa ni ya tatu
kwa ukubwa nchini India.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)