Kinondoni kuwa wenyeji wa zoezi la upandaji miti - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kinondoni kuwa wenyeji wa zoezi la upandaji miti

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko la wilaya hiyo kuhusu uzinduzi wa siku ya upandaji miti itakayofanyika kesho  kimkoa eneo la Mabwepande wilayani humo. Kauli mbiu ya siku hiyo ni 'Panda Miti, Miti ni Hazina
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

 WANANCHI wametakiwa kupanda miti na kuitunza ikiwa ni kudumisha matumizi endelevu ya misitu kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Mwito huo umetolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondono, Paul Makonda ambapo alisema maadhimisho ya siku ya kupanda miti, kauli mbiu mbiu yake ni Panda Miti, Miti ni Hazina.

Makonda alisema lengo ni kuelimisha, kuhamasisha, na kuikumbusha jamii umuhimu wa kupanda miti ambapo kilele cha maadhimisho yatafanyika mkoa Dar es Salaam, wilaya ya kinondoni, katika shule ya msingi Mjimpya kata ya Mabwepnde.

"Kila mmoja wetu anafahamu kuwa miti ina faida nyingi kwa jamii yetu ikiwemo kutupatia matunda, kivuli, dawa za asili, mapambo, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, hewa safi, kuni, mkaa na mbao,".

Alisema misitu inahifadhi wanyama pori ambao ni kivutio kwa watalii wanaotupatia fedha za kigeni hivyo kila mmoja anawajibu wa kudhamini uwepo wa miti katika mazingira yake.

Aidha Makonda alisema miti ipandwe kwa mpangilio na kuzingatia ikolojia yake, na kuifanya hamashauri ya ya manispaa ya konondoni inakuwa na madhari nzuri na kuvutia.

Alisisitiza kuwa si vizuri kupanda miti mikubwa katikati ya barabara na karibu na nyaya za umeme, ambazo zinaweza kusababisha madhara hususan katika kipindi cha mvua. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages