Kaymu yafungua tawi jipya Kariakoo - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kaymu yafungua tawi jipya Kariakoo

 Kaymu Tanzania Country Manager Erfaan Mojgani speaking to the media about the new office launched in Kariakoo which will help improve Kaymu's delivery services.
Zacharia Lucas, who has a shop on Kaymu (right) speaking to the media, about how helpful Kaymu has been in helping his business grow.(Middle) Kaymu Tanzania's country manager, (left) along with Kaymu Tanzania's Logistics and operations associate Ulumbi Bryceson.

Kaymu yafungua tawi jipya Kariakoo
Dar-es- Salaam 26.03.2015 - Kaymu Tanzania imefungua tawi jipya Kariakoo ambalo litafanya kazi kama kituo cha kuweka bidhaa kabla hazijasafirishwa kwenda katika maeneo husika. Tawi hilo jipya linatazamiwa kupunguza usumbufu ambao wauzaji walikumbana nao katika kupata huduma stahiki za kampuni.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja wa Nchi wa Kaymu Erfaan Mojgani alisema tawi hili jipya liko sambamba na mkakati wa kampuni wa kuleta huduma karibu na wauzaji.
Akiongea kuhusu ofisi hii mpya ya tawi ambayo iko Kariakoo mtaa wa Congo, Erfaan alisema, “Hii ni ishara kubwa wa ukuaji wa biashara hapa Tanzania na ni uwekezaji wa ziada nchini kuhakikisha mafanikio kwa wanunuzi na wanunuaji.”

Aliongeza, “ Tunajivunia kuwa karibu zaidi na wateja wetu; hii itasaidia sana katika mchakato wa usafirishaji bidhaa kwa kuwa tupo karibu zaidi na maduka ya wauzaji wengi. Ofisi hii inatazamiwa kutumika katika huduma za usafirishaji kila siku za kazi na pia katika kutoa huduma nyingine kama kujibu maswali ya wateja, kutoa mafunzo kwa wauzaji na kuwa na vifaa vya kutolea huduma za upigaji picha zenye ubora zaidi.

Cha Classic, moja kati ya wauzaji wa Kariakoo alisema, “Tumefurahishwa sana na hatua ya Kaymu kufungua kituo chake hapa Kariakoo. Huu mchakato mpya utatusaidia sana katika kutimiza oda zetu kwa wingi. Naamini itatusaidia katika kukuza biashara zetu.”

Kaymu inafanya kazi na wadau mbalimbali kuhakikisha bidhaa za wanunuaji na wauzaji zinasafirishwa kwa muda unaotakikana. Uanzishwaji wa ofisi mpya unachangia huduma za uhakika za usafirishaji.

Pia akiongea na vyombo vya habari Bryceson, Afisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania alisema, “Hii ni njia nyingine ya kuwasaidia wadau wenzetu wa usafirishaji bidhaa, kwa kuwa inawawezesha kuchukua bidhaa nyingi kwa wakati moja kutoka eneo moja maalum, na hivyo kupunguza ucheleweshwaji katika usafirishaji bidhaa ama kughairi kushughulikia oda kutokana na maeneo ya wauzaji husika kutokujulikana”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages