Jeshi la Wananchi nchini Tanzania limewatoa hofu watanzania kufuatia kuzuka kwa vikundi vya kigaidi vinavyodaiwa kuwapora silaha Polisi pamoja na kusababisha uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa majeshi ya Tanzania jenerali Davis Mwamunyange mara baada ya mazungumzo ya faragha baina yake na Mkuu wa majeshi ya Malawi aliyewasili nchini Tanzania Jana.
Aidha, wakizungumzia mahususiano baina ya nchi hizo wakuu hao wa majeshi wamesifu kuwepo uhusiano imara ambapo viongozi wakuu wa kitaifa pamoja na wale wa kijeshi wanapata fursa ya kutembeleana na kubadilishana mawazo.
Kwa upande wake mkuu wa majeshi ya Malawi amesema kuwa mahusiano baina ya nchi hizo hayawezi kuchukuliwa kimzaha kwa kuwa ni ya kihistoria.
Katika hatua nyingine hivi karibuni tumeshuhudia matukio kadhaa yanayohusishwa na ugaidi hasa tukio kubwa lilitokea jijini Tanga ambapo katika mapigano kati ya paolisi na kikundi cha ugaidi Mwanajeshi mmoja allifariki dunia.
Hivyo basi kauli ya Mkuu wa Majeshi ni dhahiri kuwa Jeshi hilo litasaidia katika mapambao dhidi ya vikundi vya ugaidi vinavyohatarisha usalama wa raia na mali zao.Crdt Times FM
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)