Dar es Salaam, 27 Februari 2015: Katika jioni ya umaridadi na matarajio makubwa Doreen Mashika amewageukia mashabiki wake wa bara na kuwashangaza katika usiku uliojulikana kama "Fashion Night In" uliyokuwa mjumuhisho wa rangi na miundo inayofaa kuigwa. Mbunifu huyo alowahi kushinda tuzo mbalimbali duniani alionyesha toleo jipya la mavazi yake yaliyojulikana kama “spring/summer 2015”.
Pamoja na utajiri wa vipaji alivyonavyo watazamaji walipata kuona mitindo ya kipekee, uzoefu mpya na msisimko ambayo ni alama mahususi ya Doreen Mashika Zanzibar (DMZ). Hii halikuwa tukio la kukosa lililohudhuriwa na wageni wa kimataifa kutoka maeneo mbalimbali pamoja na wanamitindo, wabunifu, watu mashuhuri na kwa ujumla wapenzi wa mitindo.
Diva wa 'Fashion Night In', Doreen Mashika alifungua onesho kwa kuonesha miundo mipya ya mtindo. Akitoa maoni juu ya mwelekeo wake wa ubunifu Doreen Mashika anasema “kama m’bunifu Najaribu kufikiri nje ya boksi na kukata minyororo ya mtazamo na iitindo iliyozoeleka, naamini ili bidhaa iweze kukubalika na kukumbukwa kweli inapaswa kuleta changamoto katika fikra za kila mmoja.
Onesho hilo ililetwa ki ubora zaidi na mkurugenzi wa uzalishaji Rob Soar kutoka London na kuwekewa muendelezo na timu yenye vipaji lukuki kutoka Dar es Salaam na Nairobi. Utanuzi huu wa lebo ya DMZ umewashangaza wafwatiliaji kwa kuchukua muelekeo mpya katika Mitindo unaozidi kuimarika na kuelekea ulimwenguni kote.
Akizungumza baada ya mtoko huo wa Doreen Mashika "Fashion Night In" Meneja Masoko wa Precision Air Services PLC Azda Nkulo alimmwagia sifa m’bunifu huyo. Alisema kuwa msaada wao katika onesho hilo umeletwa na mahusiano mazuri kati ya viongozi wa usafiri wa anga na DMZ ambapo wote katika idara zao wameendelea kuwa wa tofauti na mfano wa kuigwa, jambo linalowawezesha kuendelea kuwa imara katika soko hili dogo na linalobadilika.
Maneno ya Meneja masoko wa Precision Air yalirejewa na Eliavera Timoth, Naibu Meneja Masoko wa Toyota Tanzania Ltd. Yeye anasema kwamba "Doreen ni kijana mahiri na m’bunifu anawakilisha uzalendo wa Mtanzania wa sasa, ni mpambanaji na anayetazama kuubadili ulimwengu aliopo. Kama kampuni yenye mizizi ndani ya jamii ya Watanzania, sisi Toyota Tanzania husaidia watu kama hawa na kuamini kuwa ni wajibu wetu kwa kuwapatia jukwaa kwa ajili ya mafanikio zaidi. "
Toyota Tanzania na Precision Air waliungana na makampuni mengine ndani ya nchi ikiwemo Luxury Short Safari na Q-WAY international kupitia bidhaa zao Belvedere Vodka katika kutoa jukwaa kwa ajili ya utekelezaji wa "Fashion Night In".
Katika sekta hii ndogo na inayobadilika Doreen Mashika anakuwa kama mwanga elekezi kwa wabunifu wenzake kutokana na kujituma kwa bidii na utofauti bila kusahau utamaduni wake wa Kiafrika.
Kuhusu Doreen Mashika
Doreen Mashika alizaliwa na kukua nchini Tanzania, alisoma na kufanya kazi nchini Uswiss.
Alianza kazi katika sekta ya fedha akiwa Uswisi. Akijikita kwenye bidhaa za kifahari huko ndipo alipoanzia kupenda maswala mtindo na ubunifu. Akiongozwa kwa hisia utamaduni na utajiri uliopo barani Afrika, alirejea Tanzania na kukaa Zanzibar na kuazisha kampuni yake.
Hivi sasa, anamiliki duka lenye bidhaa zinazovutia kimataifa. Ameunda bidhaa za kipekee na kisasa zenye mchanganyiko wa mitindo ya kimagharibi na vifaa vya jadi.
Bidhaa za DMZ zinavutia rangi, mahiri na ni maridadi. Bidhaa hizo ni pamoja na viatu, mikoba, vito na nguo zinazotengenezwa kwa kutumia nguo za jadi za Kiafrika kama vile Kanga, vitenge na turubai. Katika kubuni mifuko na viatu, Mashika anashirikiana na vikundi vya wanawake kutoka vijijini wanaotengeneza vitu hivyo kwa kutumia mikono, na pia kwa kutumia mbinu za jadi za kiafrika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)