wa Tatu kutoka (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Edmund Mkwawa wa pili kutoka (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa My way Entertainment Paul Mganga,wa Kwanza (kulia) ni Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup 2015 David Manoti, wa pili (Kushoto) Samweli Mahendeka Agency Banking Manager ambaye pia ni Kapteni wa Timu ya Benki ya DCB wa tatu (kushoto) ni ni Product Development and Marketing Manager wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Boyd Mwaisame na anayemfuatia ni Chief Treasury Manager ambaye pia ni Mlezi wa Timu ya DCB Commercial Bank Plc Bw.Samwel E. Dyamo wakiwa katika Mkutano na waandishi wa Habari makao makuu ya DCB Commercial Bank Plc Leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Edmund Mkwawa akiongea na Waandishi wa Habari Makao makuu ya DCB , alithibitisha kuwa DCB Commercial Bank watashiriki katika mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup 2015 ambapo Timu yao tayari imesha anza kufanya mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo tangu mwezi wa pili mwaka huu 2015 na kuwa timu ipo katika hari nzuri sana si kwa kushiriki tuu lakini pia kutoa upinzani mkubwa watakazokutana nazo na hata kunyakua kikombe.
Pia Bwana. Mkwawa amesema kuwa DCB pamoja na kushiriki kwao lakini wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha kwa ufasaha zaidi na kuongeza kuwa lengo kubwa la DCB Commercial Bank kupitia udhamini na ushiriki wa mashindano hayo ni kupanua wigo mkubwa wa kimahusiano na kibiashara kwa ukaribu zaidi baina ya Benki,Mifuko ya kijamii na Jamii kwa ujumla. Mwisho alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kufika katika viwanja ambapo mashindano yatafanyika ili kujipatia Huduma Bora za Benki ya DCB na kujiunga na huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo katika Banda lao maalum ambalo litakuwa katika viwanja hivyo.
Pia Bwana. Mkwawa amesema kuwa DCB pamoja na kushiriki kwao lakini wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha kwa ufasaha zaidi na kuongeza kuwa lengo kubwa la DCB Commercial Bank kupitia udhamini na ushiriki wa mashindano hayo ni kupanua wigo mkubwa wa kimahusiano na kibiashara kwa ukaribu zaidi baina ya Benki,Mifuko ya kijamii na Jamii kwa ujumla. Mwisho alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kufika katika viwanja ambapo mashindano yatafanyika ili kujipatia Huduma Bora za Benki ya DCB na kujiunga na huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo katika Banda lao maalum ambalo litakuwa katika viwanja hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa My Way Entertainment Bw. Paul Mganga akiongea na waandishi wa Habari Makao makuu ya DCB Commercial Bank leo, alisema kuwa wanatarajia kuwa na mwitikio Mkubwa wa Taasisi za Kifedha na Mifuko ya Jamii katika Mashindano ya Tanzania Bankers Cup and Public Funds Cup kwa kujiunga na mashindano haya kama ilivyo DCB Benki ambao wameweza kuwa wa kwanza kuthibitisha wanashiriki mashindano hayo na Kudhamini pia na kuwashukuru kwa hilo, alihimiza kuwa Taasisi zengine za Kifedha na Mifuko ya Kijamii kuwa na mwitikio mkubwa wa mashindano hayo, kwani Michezo hujenga afya Bora na kukuza akili kama ilivyo kauli mbiu ya Mashindano haya"Tuungane katika Michezo, Michezo ni Afya , Michezo ni Ajira" Mwisho aliishukuru Benki ya DCB kuonesha mwamko mkubwa katika Swala la Michezo na kuomba Taasisi nyengine za Kifedha na Mifuko ya Jamii kuwa na mwamko huo.
Product Development and Marketing Manager wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Boyd Mwaisame akisisitiza Jambo wakati wa Mkutano huo wa Benki ya DCB na waaandishi wa Habari juu ya Mashindano ya Tanzania Bankers and Public Funds Cup alisema kuwa ndani ya viwanja vya michezo kutakuwa na Banda maalum la DCB Commercial Bank ambapo huduma mbalimbali za Benki hiyo zitatolewa eneo hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Tanzania Bankers and Pensions Funds Cup 2015 Bw. David Manoti alitoa wito kwa vyombo vya habari , wadau wa Michezo, na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya yatakayofanyika katika viwanja vya wazi ili kuweza kujionea burudani ya pekee itakayokuwa inaendelea katika viwanja hivyo.
Mkutano na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Benki ya DCB juu ya Ushiriki wao na Kudhamini mashindano hayo ukiwa unaendelea ambapo Mashindano hayo yanatarajia kuanza Rasmi 28 Machi 2015.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)