NA MWANDISHI WETU
UPANDE wa utetezi katika kesi iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara Hans Macha, umesema Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetenda haki kwa kuthibitisha kuwa mteja wao alinunua nyumba kihalali kutoka kwa mlalamikaji Ramadhani Balenga.
Kauli hiyo ya upande wa utetezi, imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Devotha Kisoka kutoa hukumu iliyothibitisha kwamba Macha alinunua nyumba kihalali kutoka kwa Balenga.
Wakili wa Macha, Deo Ringia alidai mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam, kwamba mahakama hiyo imetenda haki kwa sababu ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulikuwa na mashaka na wa kuunga unga.
Alidai kwa upande wao, wamepokea hukumu hiyo kwa furaha zaidi kwani haki imetendeka.
"Haki imetendeka na mteja wetu amepumua. Tumeipokea hukumu kwa furaha zaidi kwani haki imetendeka kwa sababu hata usahahidi wa upande wa Jamhuri ulivyokwenda ulikuwa na mashaka na wa kuunga unga," alidai.
Wakili Ringia alidai atazungumzia zaidi hukumu hiyo ambayo Hakimu Moshi aliisoma kwa kifupi, baada ya kupata nakala yake.
Novemba, mwaka jana, mahakama hiyo ilimuona Macha ana kesi ya kujibu na kutakiwa kuwasilisha utetezi wake, baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake.
Macha wakati akijitetea aliita mashahidi takriban 10 ambapo, alikanusha tuhuma hizo kwa madai ni za uongo na kuiomba mahakama kuyatupilia mbali mashitaka hayo.
Alidai tuhuma hizo ni za uongo kwa sababu Balenga anafahamu kwamba alimuuzia nyumba hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)