Vituo vitatu vya Kenya vyasitisha matangazo yao
Kampuni tatu kubwa za kibinafasi za utangazaji zimesitisha kupeperusha matangazo kwenye televisheni kwa muda wa siku tatu zilizopita,
baada ya serikali kudhibiti mitambo ya zamani ya kupeperusha matangazo kwa mfumo wa analojia.
Kampuni hizo za Standard Media, inayomiliki runinga ya kwanza ya kibinafsi nchini Kenya KTN Nation media Group inayomiliki NTV na QTV
na Royal Media Services inayomiliki Citizen TV zimekuwa katika malumbano makali na serikali kuhusu uhamiaji wa kupeperusha matangazo kwa kutumia mfumo wa digitali kutoka ule wa zamani analojia.
Runinga hizo tatu zimekuwa zikilumbana na halmashauri ya serikali ya mawasiliano kuhusu swala la kuhama kutoka mfumo wa zamani hadi digitali kwa zaidi ya miaka nne sasa.
Hatua ya mwsihoni mwa wiki ya kufunga mitambo ya zamani ya kurushia matangazo yaani analogue ya runinga hizo ilichukuliwa baada ya amri ya mahakam ya juu zaidi nchini Kenya kuidhinisha uhamiaji huo.
Wamiliki wa runinga hizo tatu wanasema hawajajiandaa vilivyo kwa uhamiaji huo.
Lakini, je, nini hasa chimbuko la vyombo hivyo tatu vya habari kusitasita katika uhamiaji huu wa digitali?
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari vya Kenya anasema kuwa Serikali ilipendelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na wageni na hivyo kuwanyima fursa wakenya kumiliki na kuchangia katika ukuaji wa
sekta ya utangazaji nchini Kenya.
Kwa sasa, watazamji wanategemea sana vituo viwili vikubwa, kile cha K24 ambacho kinadaiwa kumilikiwa na familia ya rais wa Kenya na runinga ya kitaifa ya shirika la utangazaji la Kenya.
Kwa upande wake, serikali ya Kenya kupitia halmashauri ya mawasiliano CAK inasisistiza kwamba zaidi ya wakenya asilimia 60 wanavyovijisanduku vipya vya kuwawezesha kupokea matangazo kwa njia ya digitali.
Katika mitaa ya mji mkuu wa Nairobi, baadhi ya wakenya wanaelezea jinsi walivyokosa kutizama vipindi vyao wanavyovipenda.
Hata hivyo wengine wanakubaliana na serikali kuwa sharti mipango ya serikali ya kuhamishwa kwenye masafa ya kidijitali yaendelee mbele ilikufungua sekta nzima ya sanaa.
Kulingana na sera za serikali ya Kenya runinga zote zinahitajika kuandaa na kupeperusha asilimia 60% ya vipindi kutoka nchini Kenya huku asilimia 40 ikiwa vipindi kutoka ughaibuni.
Wakenya wengi wanahisi kuwa serikali iliharakisha uhamiaji huo ila wangependa sekta nzima ifuate sheria za nchi.
Mnano mwaka wa 2006, kongamano la kimataifa kuhusu mawasiliano lililoandaliwa mjini Geneva Switzerland liliazimia kwamba nchi wanachama ziwe zimehama kutoka mfumo wa zamani wa utangazaji wa analogue hadi digitali
ifikapo tarehe 17 mwezi juni mwaka wa 2015.
Ingawa tarehe hiyo bado haijawadia, mamilioni ya watazamji wanaotegemea runinga za KTN, NTV na Citizen tayari wanaonja athari za kukera za maendelezi ya teknologia.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)