Wanasayansi wanakadiria kuwa inagharimu zaidi ya dola
za marekani trilioni elfu sita kuiga tishu na viungo vya mwili wa binadamu.
Gharama hiyo ni mara 77 ya pato la dunia. Pamoja na gharama hii yote, hakuna
hakikisho kwamba jambo hili litafanikiwa. Gharama hii haijumuishi akili
aliyojaaliwa binadamu. Hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na mwanasayansi Harold
J. Morowitz wa chuo kikuu cha Yale nchini Marekani.
Nchini Tanzania kuna ongezeko kubwa la kuenea kwa
magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha. Magonjwa hayo ni pamoja na kiharusi,
ugonjwa wa ubongo, pumu, ini, kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kufeli kwa
figo, kupooza, msongo wa mawazo, uzito na unene uliopitiliza, shinikizo la
damu, saratani, magonjwa sugu ya mapafu (COPD), matatizo ya kusikia, maumivu sugu
ya mgongo na mengine mengi. Kila mwaka, kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo linalosababishwa
na magonjwa haya ambayo ni rahisi sana kuzuilika. Huu ni wakati muafaka wa kubadilisha hali hii.
Maradhi mengi ya aina hii yanayotokana na jinsi
tunavyoendesha maisha yetu ya kila siku. Mlo wetu na maisha kwa ujumla ndio
chanzo kikubwa cha magonjwa haya. Watanzania wengi hutumia nyama kwa wingi, mafuta
ya mboga, vyakula vya makopo, tumbaku, madawa, pombe na vyakula vyenye sukari.
Wengi wetu tumechagua maisha ambayo yanaongeza uzito na unene uliopitiliza na
mwili usiokuwa na mazoezi. Mabadiliko haya yamechangia kwa kiasi kikubwa magonjwa
kama saratani ya utumbo, saratani ya tezi dume, saratani ya matiti, saratani ya
mapafu na saratani nyinginezo.
Nchini Tanzania Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
imeanzisha Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya Namba III wa mwezi Julai 2009 hadi
Juni 2015 ambao unatoa wito kwa ajili ya mabadiliko ya mitindo mbaya
wa maisha kwa kiasi kikubwa ili kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha yake.
(I) Kulingana na mpango mkakati huo, watu lazima
wawezeshwe ili kubadilisha mfumo wa maisha yao na kuchagua maisha mazuri
kwaajili ya afya zao. Sekta ya afya
inalenga uwezeshaji kwa watu binafsi,
familia na jamii ili kuboresha maisha, kwa njia ya Majadiliano juu ya
mabadiliko ya Tabia. Kushirikiana kwa wadau katika mashirika ya kiserikali na
yasiyo ya kiserikali ni muhimu katika suala hili ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya
kuambukiza.
Wakati tukihadhimisha Siku ya Saratani Duniani, Dk
Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORIC)
alinukuliwa akisema kwamba wagonjwa wengi wa magonjwa ya kansa husababishwa na
mtindo wa maisha ya sasa. Belinda Liana, Afisa Mwandamizi wa Mpango (Lishe),
Kituo cha Ushauri, Lishe na huduma za afya (CONSENUTH), anatoa wito kwa
Watanzania kubadilisha maisha yao kama njia moja ya kupunguza uwezekano wa
kupatwa na magonjwa kwa ujumla. Anasema
"watu wanapaswa kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta ikiwa ni pamoja
na chips, protini hasahasa nyama nyekundu na vitu sukari"
(ii) Kutokana na maisha mabovu ambayo wengi wetu
tumeyachagua, Madaktari duniani kote wameguswa na hali hii na kuamua kuonya juu
ya maradhi yanayochangiwa na mtindo wa maisha. Hospitali za Apollo ni mmoja wa
hospitali zinazohamasisha maisha yenye afya bora.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dk.
Prathap .C. Reddy anasema kuwa, "Uhai ni kitu kisichoweza kununulika na
afya njema ni zawadi ya thamani sana kwetu! Afya njema ya mwili na akili
inatusaidia kuishi maisha safi, na kufurahi wakati wote. Hivyo basi afya njema ni
kitu ambacho tunakihitaji wakati wote". (iii)
Anaongeza kuwa "Mwenyezi Mungu katujaalia mwili
wenye afya nzuri, ambao haujatugharimu hata kidogo. Mwili wetu ni wa thamani
sana, lakini kwa bahati mbaya wengi wetu hatuuchukulii hivyo. Tunatakiwa
kuthamini mwili wetu, kuulinda na kuuenzi pia. Muhimu zaidi ni lazima kuupatia
heshima unayostahili. Tunajua cha kufanya ili tuwe na afya njema lakini
hatufanyi. Matokeo yake yanajidhihirisha sasa tumekuwa na afya mbovu
iliyosheheni magonjwa. "
Anamalizia kwa
kusema kwamba, “Hata sasa, tunasogeza huduma za afya kwenda ulimwengu wa
‘huduma za afya kwa kila mmoja’ ambayo inahusiana na maumbile tofauti ya watu
tofauti. Tunafanya hivi ili kurahisisha uchunguzi bora, matibabu na kinga bora
na makini zaidi. Ila hiyo haitoshi. Kwa sisi kuwa na afya bora jambo la muhimu
zaidi ni hili; unapaswa kudhibiti afya yako. Unapaswa kuelewa kuwa Afya
yako hainunuliki, na kuutendea mwili wako unavyopaswa kutendewa. Tuufanye mwaka
huu kuwa wa uponyaji, na siyo tu kutibiwa.
Hii inathibitisha
ni kiasi gani tunahitaji kuwa makini kuhusu kuwa na afya njema na kufanya jambo
hili liwe kipaumbele chetu. Kama unataka kuepukana na magonjwa ya mtindo wa
maisha, ni muhimu kuzingatia mlo kamili kwa afya na mazoezi ya mara kwa mara.
Afya njema inaanza kwa Kujizoeza kuupa mwili vitu vyenye umuhimu kwake. Afya
bora ni hatua ndogo zinazotusaidia kupiga hatua kubwa kuelekea mbele. Uhai
haununuliki. Tujitahidi kuishi kulingana na thamani yake halisi.
Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali
ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa
ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa
karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika
elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".
Katika
miaka 30 tokea kuanzishwa kwake,
hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni
moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi
makubwa katika sekta ya afya nchini india.
Katika
safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi
120.
Inatoa
huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710
Imefanya
upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za
mishipa myembamba.
Imefanya
upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa
uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.
Taasisi
ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za
kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)