Wananchi waliojitokeza katika sherehe ya makabidhiano ya vitabu milioni 2.5 vya sayansi na hisabati kwa shule za sekondari za serikali nchini. Vitabu hivyo kutoka serikali ya watu wa Marekani vilikabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress katika hafla iliyofanyika Shule ya Sekondari Mtakuja Beach iliyopo Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam leo. Hafla hiyo ilifanyika katika shule hiyo kwa niaba ya shule zote za serikali nchini.
Rais Jakaya Kikwete na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja Beach huku wakiwa wameshika baadhi ya vitabu walivyokabidhiwa katika sherehe hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi vitabu hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akihutubia
kwenye hafla hiyo.
Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni ambayo ilikuwa mwenyeji wa sherehe hizo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kushoto), akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete sehemu ya vitabu ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya vitabu milioni 2.5 vya sayansi na hisabati vilivyotolewa na serikali ya Marekani kwa ajili ya shule za sekondari za serikali nchini katika hafla iliyofanyika Shule ya Sekondari Mtakuja Beach iliyopo Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam leo. Hafla hiyo ilifanyika katika shule hiyo kwa niaba ya shule zote za serikali nchini. Vitabu hivyo tayari vimesambazwa katika shule hizo nchini.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja Beach wakishangilia katika sherehe hiyo.
Wanawake wakicheza wimbo wa Christian Bela wa Mama.
Wadau wa elimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanawake wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete
akiwasili kwenye sherehe hizo.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiteta jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa wakati wakimsubiri Rais Kikwete awasili.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda (kulia), akitoa taarifa ya shughuli za maendeleo katika sekta ya elimu mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakitoa burudani katika hafla hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)