Marehemu Andrew Michael Kumalilwa enzi za uhai wake
Familia ya Bwana Andrew Michael Kumalilwa inasikitika kutangaza kifo cha wa baba yao mpendwa Bwana Andrew Michael Kumalilwa kilichotokea tarehe 09 Februari 2015 Jijini Dar Es Salaam.
Marehemu Andrew Michael Kumalilwa alizaliwa mnamo tarehe 10 Machi 1938 na aliwahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwepo ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCP) na msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea na Mazishi yatafanyika Kesho Nyumbani Kwake Segerea.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina
Timu nzima ya Lukaza Blog inapenda kutoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wao. Mungu awatie nguvu katika Kipindi hiki Kigumu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)