News Alert: Jengo lililopo mtaa wa Jamhuri na Mosque Jijini Dar lawaka Moto - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

News Alert: Jengo lililopo mtaa wa Jamhuri na Mosque Jijini Dar lawaka Moto

Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Jamuhuri na Mosque jijini Dar es salaam na kuteketeza  mali kadhaa. Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha
moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la
tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto
nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Jamuhuri na moski.
 Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari  la zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio hivi punde.Kwa Hisani ya Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages