Mugabe kufanya sherehe ya kutimiza miaka 91 kesho - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mugabe kufanya sherehe ya kutimiza miaka 91 kesho

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kesho atafanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 91 kwa kuchinja tembo wawili.
Sherehe hizo zitafanyika kwenye mji wa Victoria Falls na zinaandaliwa na chama tawala ZANU-PF kinataka kukusanya dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya sherehe ya kesho. Wageni wapatao 20,000 wanatarajiwa kuhudhuria.
Hata hivyo, mashirika ya kutetea ulinzi wa wanyama pori yamemkosoa Mugabe, wakisema haiwezekani akakemea uharamia wakati yeye mwenyewe anaamuru wanyamapori wachinjwe.
Pamoja na hayo baadhi ya raia wa Zimbabwe wanakerwa na uamuzi wa rais wao kufanya sherehe kubwa kama hiyo, wakati wananchi wake wengi ni maskini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages