Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo utafanyika siku ya Alhamisi Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Burundi
Ujumbe wa Kenya
Ujumbe wa Uganda na Rwanda
Mkutano ukiendelea.
Balozi wa Tanzania nchini Martekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
Mkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika leo siku ya Jumatano Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.
Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi,
Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi MFA & IT Kenya, Bi. Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir PA to CS MEACT Kenya.
Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred Nwam na Stilson Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.
Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)