Makamu Wa Rais Dkt Bilal ashirikiana na wananchi wa Mkoa wa Dar katika mazishi ya wanafamilia waliopoteza maisha katika ajali ya Moto - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Makamu Wa Rais Dkt Bilal ashirikiana na wananchi wa Mkoa wa Dar katika mazishi ya wanafamilia waliopoteza maisha katika ajali ya Moto

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali leo amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliofuruka kuwazika ndugu wa familia moja wapato 6 waliofariki katika ajali ya moto iliyoteketeza nyumba yao. 

Pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na viongozi wengine mbalimbali wa kitaifa walishiriki mazishi hayo akiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark Mwandosya ambaye ni mwanafamilia hiyo. 

Waliofariki katika ajali hiyo ni Kapteni mstaafu wa JWTZ, David Mpira na Mkewe Selina Yegela watoto wao Lucas Mpila na Samwel Yegela na wajukuu Selina Emmanuel (9) na Pauline Emmanuel (3).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto nyumbani kwao Kipunguni, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga, Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam. 
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakishusha masanduklu yaliyo hifadhi miili hiyo ya marehemu.
 Watoto kutoka Kanisa Katoliki Ukonga wakipita kutoa heshima.
 Askofu akiweka udongo katika makaburi hayo Ukonga Airwing Dar es Salaam.
 Waombolezaji wakifukia makaburi 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye makaburi ya familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Air wing Ukonga Dar es salaam.
Waombolezaji wakiwa msibani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages