Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah (kulia) na Kiongozi wa Skauti, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha Nishani ya Juu, Skauti Barnaba Abel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015. Kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah na (kulia kwa Makamu) ni Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah (kulia) na Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia kwa Makamu) wakisimama kupokea maandamano ya Vijana wa Skauti, yalipokuwa yakiingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, leo Feb 21, 2015.
Vijana wa Skauti wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa maandamano wakati wa sherehe hizo za maadhimisho hayo. Picha na OMR
Vijana wa Skauti wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa maandamano wakati wa sherehe hizo za maadhimisho hayo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi na Skauti wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, zilizofanyika leo Feb 21, 2015 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Skauti baada ya sherehe hizo. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)