Pages

Makamu wa Rais Dkt Bilal afungua Kongamano la Kimataifa la Watoto waishio katika Mazingira hatarishi

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid machapisho mbalimbali baada ya kuzindua kongamano la siku mbili la kimataifa la watoto walio katika mazingira hatarishi Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba machapisho hayo.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki machapisho hayo kwa niaba ya wakuu wote wa mikoa.
Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (Unecef), Mbelwa Gabagambi, akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa World Vision, Devocatus Kamara akizungumza na waandishi wa habari.
Mwakilishi wa watoto, Coletha Emanuel kutoka mkoani Shinyanga akisoma hutuba yao mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal.
Wadau wa maswala ya watoto wakiwa kwenye kongamano hilo.
Watoka kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye 
kongamano hilo.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi wa kongamano hilo.
Wapiga picha za habari wakichukua matukio ya kongamano hilo.
watoto wakiwa kwenye kongamano hilo.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati waliokaa mbele na viongozi wengine), wakiwa katika picha ya pamoja na watoto walioshiriki katika kongamano hilo kwa niaba ya wenzao.

Mwenyekiti wa Ulinzi wa Usalama wa Mtoto Kata ya Mabwepande, Mwanne Yusuf Msekalile, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Shirika la World Vision lilivyowasaidia kuhusu maswala ya ulinzi na usalama wa watoto.
Wanamuziki wa Mjomba Bendi wakitoa burudani katika hafla ya kuzindua kongamano la siku mbili la kimataifa la watoto.

Dotto Mwaibale

WATOTO wamuomba Rais Jakaya Kikwete kutilia mkazo mabadiliko ya sheria ya watoto itakayokomesha vitendo vya kikatili dhidi yao.

Pia wamemuomba Rais kuweka msisitizo katika upatikanaji bure wa huduma za afya na pamoja na huduma za msaada wa kisheri.

Hayo ameyasema Dar es Salaam leo Mwakilishi wa watoto, Colletha Wilfred, katika hafla ya  ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Ustawi wa Watoto.

Akizungumza katika ufunguzi huo Coletha alisema kuwa yapo makundi mbalimbali ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo ni watoto wanaoishi na Virusi vya Ukimwi,Yatima na watoto ambao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia kama kulawitiwa na kubakwa.

Mtoto huyo alisema kuwa makundi hayo yote ni wahanga wakubwa wa ukatili hivyo wanamuomba Rasi kuweka mkazo katika marekebisho ya hseria za watoto.

Aidha alisema watoto wamekuwa wakikosa huduma za kiafya pindi wanapofanyiwa ukatili hivyo hilo nalo serikali lilione ili watoto hao waweze kupatiwa huduma bila gharama yoyote.

Wilfred alisema kuwa serikali iangalie sheria ya makosa ya jinai kama ubakaji na ulawiti, kwani iliyopo inawaoa haki washatikiwa kupata dhamani jambo ambalo linachangia watoto kupata vitisho kutokana na kutoa sheria.

Aliongeza kuwa si serikali peke yake inatakiwa kuwa waangalizi wa watoto hao bali ni jukumu la kila mtanzania kuwasaidi.

Mbali na hayo alisema kuwa ni matumaini yao kuwa Rais amesikia kilio chao na atafanyia kazi yale yote waliyomueleza katika kunusuru maisha ya watoto nchini.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal alisema kuwa ni ukweli kuwa hali ya usalama wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni mbaya na inatisha.

Dk Bilali alisema kuwa Umasikini,Ukimwi,Ukatili na Unyanyasaji unachangia ongezeko la watoto wanaoishia katika mazingira magumu na kufikia 897,913.

''Utafiti unaonesha kati ya watoto 10 wakike watoto 3 lazima wafanyiwe vitendo vya kikatili na kati ya watoto 7 wakiume mtoto moja lazima awe muhanga wa ukatili, hii hali inatisha sana na inaonesha kuwa watoto hawapo katika usalam."alisema

Hivyo alisema kuna kila sababu ya kuumiza vichwa kukomesha tatizo hilo na wao kama serikali wamesikia na watatekeleza kilio cha watoto hao.

Alisisitiza kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo ya watoto kwa kushirikiana na wadau ili kila mtoto kuishi maisha bora na salama.

Pamoja na hayo Waziri wa Afya, Dk. Rashid Seif alisema jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuwasaidia watoto wanaoishi maisha magumu kupitia misaada ya kisheria.

Dk. Rashid alisema kuwa jumla ya watoto 2,332 ambao walikuwa katika ajira za utotoni walipatiwa huduma za misaada ya kisheria na kundokana na ajira hizo.

Alisema kuwa takwimu la zoezi la halmashauri 110 la utambuzi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu ilionesha kuwa jumla ya watoto wa kiume 475,000 na jumla ya watoto wa kike 571,000 wanaishi katika mazingira magumu. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)