Sekta ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi
yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi,
njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya. Teknohama
imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni
yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika
kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara
makubwa kwa mgonjwa.
Kuna
matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii
ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu
yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia
roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida,
au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu
inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.
Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta
inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Hudhibiti huu ni sawa na
ule wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa
usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa
ikitumika awali ya ‘laparoscopic’.
Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe tata
pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda
mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya
uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.
Upasuaji kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu
hali mbalimbali kama vile magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja
kuondoa mfuko wa uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani
katika mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe
kwenye mfuko wa uzazi (fibroids uterine), saratani ya shingo ya kizazi,
saratani ya mfuko wa kizazi, fistula na viungo
katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed). Utaratibu wa upasuaji na
ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi kupitia teknolojia hii. Kulingana
na huduma ya afya inayoitajika na umri wa mgonjwa, upasuaji kutumia Roboti pia
unaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo wa kuzaa.
Kwa wagonjwa wa Saratani, mara nyingi upasuaji wa aina
hii huusisha upasuaji wa kichwa, shingo,
ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake, kuondoa uvimbe kwenye utumbo (colorectal
surgery) na upasuaji unaohusisha nyonga.
Mfumo huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa
ambao wanahitaji upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini
ya shingo. Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila
kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.
Mwaka 2012 Ashura Ibrahim, msichana mwenye
umri wa miaka saba kutoka Tanzania alipewa nafasi nyingine katika maisha
kupitia upasuaji kwa kutumia Robot. Mwaka 2010, mtoto huyo alipata ajali
iliyohusisha Bajaji na gari mjini Dar-es-Salaam, janga hilo ilisababisha kuharibiwa
kwa kibofu chake. Pamoja na upasuaji kadhaa uliofanyika nchini, matokeo hayakuridhisha.
Kwa msaada kutoka Wizara ya Afya na usitawi wa jamii, Ashura alipelekwa hospitali
ya watoto ya Apollo mwaka 2011, ambapo alifanyiwa upasuaji kuimarisha kibofu cha
mkojo. Hata hivyo, akarudi baada ya mwaka, madaktari wakagundua kwamba akiwa
katika hatua za uponyaji, mrija wa mkojo wa upande wa kushoto ulikuwa umeshuka
chini isivyo kawaida, na kusababisha mkojo kurudi kwenye figo. Hii ingeweza
kusababisha uharibifu wa figo au maambukizi yanayosababishwa na mkojo.
Dk. Sripathi alisema kwamba upasuaji wa
kawaida usingeweza kufanyika, kwa vile alikuwa tayari amefanyiwa upasuaji mara
kadhaa. Ilibid afanyiwe upasuaji aina ya ‘Laparoscopic’, lakini huu pia
haukuweza kufanyika kwa sababu kufanya kazi kwa kutumia vyombo viwili vigumu
ilikuwa sio vizuri kiutaratibu, hivyo chaguo la mwisho ilikuwa kutumika kwa Da
Vinci robot. Upasuaji uliochukua muda wa masaa matatu kwa kutumia mikono maalumu
ya robot, na bila kupasua upya kibofu cha mkojo, mirija hiyo iliweza kurudishwa
sehemu yake ya kawaida.
Upasuaji huo ulimuacha mtoto Ashura na majeraha
madogo sana kwenye tumbo lake. Dr Sripathi aliongeza kuwa upasuaji huu ni wa
kwanza ukihusisha kibofu cha mkojo, na kwamba tatizo hilo limeondolewa siku
moja tu na hakuna damu iliyokuwa ikionekana katika mkojo baada ya upasuaji.
Dk. Rooma Sinha, Mshauri Mwandamizi wa magonjwa ya
wanawake, na upasuaji katika hospitali ya Apollo; Hyderabad nchini India,
ameelezea faida ya upasuaji kwa kutumia Roboti. Anasema kuwa,
"teknolojia ya kutumia Robot katika upasuaji itadumu sana kama tunaweza
kuona faida nyingi za teknolojia hii ikilinganishwa na njia mbalimbali za
zamani za upasuaji. Ni hatua ya pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu
huku ukiangalia kwenye Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja ya
kufanya upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi ".
Anaongeza kuwa, "Upasuaji wa kutumia Robot ni njia mpya
ya upasuaji ya isiyo na madhara na inajumuisha upasuaji wa kawaida (Open
surgery) na Upasuaji wa kutumia skrini ya computer (laparoscopic). Kwa msaada
wa Mikono maalumu ya Robot inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya upasuaji
kupitia mikato midogo sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na makovu
makubwa yatokanayo na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu, maumivu
baada ya upasuaji na kupona kwa haraka zaidi ".
Mwaka jana, Hospitali Apollo mjini Hyderabad
imefanikiwa kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna
shaka kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kiungo muhimu katika masuala ya
upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi zinazoendelea.
Kuhusu Hospitali ya
Apollo
Hospitali
za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa
kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara.
Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee
katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Taasisi
ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa
huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa.
Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
Mfumo huu wa
upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na
mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na
magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)