Leo katika kujifunza kuhusu matairi ya gari lako tunaangalia kitu kinaitwa upepo. Wote nadhani tunafahamu kuwa matairi yawe ya tube au tubeless yanahitaji kujazwa upepo ili kuweza kufanya gari litembee vizuri barabarani na kwa spidi stahiki lakini bila hivyo gari halitaweza kutembea barabarani kwa staili inayohitajika.
Leo tunaangalia ni kiasi gani cha upepo kinachohitajika kujazwa katika matairi ya gari yako.
Kwa kuanza tunapenda kusema kuwa ujazo wa upepo kwenye tairi haufanani na hii inatokana na utofauti wa makampuni ya utengenezaji wa magari na aina ya magari kampuni hizo ya utengenezaji wa magari huweka viwango tofautitofauti kutokana na aina ya magari wanayotengeneza kama Ukubwa wa gari, mzunguko wa matairi katika aina za magari, na Uzito wa gari likiwa tupu au likiwa limebeba watu au mizigo.
Utawezaje kujua ujazo sahihi wa upepo katika matairi ya gari lako.
Hii ndio alama inayotumia kwa ujazo wa upepo katika tairi PSI utakuta sehemu imeandikwa 50 psi, 35psi nk. Popote uonapo kitu kama hiko jua huo ndio ujazo sahihi wa tairi la gari lako.
Kwanza matairi yote yale ambayo yanatumika katika magari huwa yana maelezo yote muhimukatika tairi husika na unachotakiwa kufanya ni kusoma maelezo yote ambayo yameandikwa katika tairi na maandishi hayo hayapo kama mapambo tu hapana yapo kwaajili ya kuelezea kila kitu kinachihusiana na tairi.
Vilevile unaweza kuangalia kupitia kitabu cha gari, au kwenye upande wa dereva ndani au magari mengine yanakuwa yameandikwa katika mkanda.
Kutokujaza kipimo sahihi cha upepo hupelekea madhara ya kupunguza uhai wa tairi lako kwa silimia 25 na kusababisha ulaji wa mafuta katika gari kuongezeka kwa asilimia 5 zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)