Ivory Coast yatinga fainali ya AFCON 2015. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ivory Coast yatinga fainali ya AFCON 2015.

Timu ya Ivory COast imeweza kufuzu kuingia katika fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa AFCON baada ya kuichapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo magoli 3 kwa 1 katika mchezo wa kwanza wa Nusu fainali ya kwanza iliyochezwa jumatano usiku katika Mji wa Bata.

Katika mchezo huo Nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure aliwanyanyua mashabiki wa Ivory Coast kwa kuifungia timu yake goli la kwanza katika Dakika ya 20 kutokana na Mkwaju mkali na kumfanya mlinda mlango wa Congo Kidiaba asijue la kufanya.
Dakika ya 24 timu ya Congo ilipata bao la kusawazisha lililofungwa na Mchezaji Mbokani Bezua kwa mkwaju wa penati.
Gervinho akafunga bao la pili katika dakika ya 41. Hivyo hadi mapumziko Ivory Coast ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana. Wilfried Kanon alikamilisha sherehe kwa timu yake ya Ivory Coast alipofunga bao la tatu katika dakika ya 68. Kwa matokeo hayo Ivory Coast imetinga fainali za michuano ya Afcon mwaka 2015, ambapo inamsubiri mshindi wa nusu fainali ya pili, kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea, Alhamisi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages