BABA WA MSANII DULLY SYKES AFARIKI DUNI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BABA WA MSANII DULLY SYKES AFARIKI DUNI

BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Dully Sykes, mzee Ebby Sykes amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Presha.

Ebby Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae Dully Sykes.

Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka huu alikuwa anatimiza miaka 63.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

-Amen

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages