500 waokolewa machimboni Afrika Kusini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

500 waokolewa machimboni Afrika Kusini

Mchimbaji akiokolewa na wafanyakazi wa kitengo cha zimamoto
Inakadiriwa kuwa wachimbaji wapatao mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya madini nchini Afrika Kusini.
Moto mkubwa uliripuka mapema mwanzoni mwa wiki hii umbali wa zaidi ya kilomita mbili katika machimbo ya mgodi wa Kusasalethu Magharibi mwa mji wa Johannesburg.
Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo .
Moto huo unasadikiwa ulianza wakati wa kazi ya matengenezo ilipokuwa ikiendelea.
Mwaka wa jana mgodi huo ulifungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuwaondoa wachimbaji haramu ambao waliuvamia mgodi huo ambao wanshukiwa kuwa wao ndio walioanzisha moto huo.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages