SWITZERLAND YAPOKEA KICHAPO CHA SPAIN KUTOKA KWA UFARANSA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SWITZERLAND YAPOKEA KICHAPO CHA SPAIN KUTOKA KWA UFARANSA.

Mfungaji bao la Ufaransa Benzema
Ufaransa imejikatia tikiti ya kusonga mbele ikiongoza kundi E licha ya kuwa na mechi moja imesalia dhidi ya Equador .

Switzerland imebakia ya pili ikiwa na alama tatu na hivyo hainabudi kushinda mechi yao ijayo dhidi ya honduras kujihakikishia nafasi katika 16 bora.
Timu hiyo ya Ufaransa iliyoishinda Honduras 3-0, katika mechi yao ya ufunguzi, iliiangamiza timu ya Uswisi iliyokua na sifa ya kutoshindwa katika michuano kumi, ya kombe la dunia.
Olivier Giroud alifunga bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya kumi na saba naye Blaise Matuidi akafunga la pili sekunde chache baadaye
Karim Benzema alipewa penalti lakini mkwaju wake ukazuiwa na kipa wa Uswisi, Diego Benaglio.
Yohan Cabaye aliurudisha mpira baada ya kuokolewa na Benaglio, ila uligonga juu ya lango la Uswisi.
Ufaransa waliongeza bao la tatu kabla ya muda wa mapumziko.
Bao la Benzema lafutiliwa mbali lakini ufaransa inailaza Uswisi 5-2

Olivier Giroud alimpa Mathieu Valbuena pasi safi baada ya kona ya waswisi. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages